Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vigogo kikaangoni baraza la maadili

Jaji mstaafu, Sivangilwa Mwangesi,

Dar es Salaam. Viongozi wawili wa umma wanakabiliwa na tuhuma za ukiukaji wa maadili ya viongozi wa umma na tayari Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, imepokea malalamiko hayo na kuyapeleka kwenye Baraza la Maadili.

Viongozi wanaokabiliwa na tuhuma hizo ni Mathew Mbaruku ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga pamoja na Julius Ningu, Mkuu wa Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Septemba 4, 2023 na Kamishna wa Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji mstaafu, Sivangilwa Mwangesi, viongozi hao wanatuhumiwa kwa ukiukaji wa maadili kwa mujibu wa kifungu cha 6 na 12 vya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Namba 13 ya mwaka 1995.

“Baraza la Maadili linatarajia kufanya kikao cha uchunguzi wa kina wa malalamiko hayo kwa mujibu wa kanuni ya 11 ya Kanuni za Maadili ya Viongozi wa Umma (Mwenendo wa Uchunguzi wa Malalamiko katika Baraza la Maadili) za mwaka 2017,” alisema Mwangesi kwenye taarifa hiyo.

Alisisitiza kwamba kikao hicho cha uchunguzi kinafanyika leo kuanzia saa 3:00 asubuhi na kitamaliza kesho, jijini Dodoma katika ukumbi wa mikutano ulioko katika ofisi ya mkuu wa mkoa.

Jaji mstaafu Mwangesi, alisema katika taarifa yake kwamba uchunguzi huo wa wazi unafanyika kwa mujibu wa kifungu cha 25 (5) na 29 (6) cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma (Sura 398).

“Wananchi wote mnaalikwa kuhudhuria katika kikao hicho muhimu,” alibainisha Jaji Mwangesi kwenye taarifa yake iliyotolewa jana kwa umma.