Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Utovu wa maadili chanzo cha rushwa nchini

Muktasari:

Imeelezwa kuwa kukosekana kwa maadili katika ngazi ya familia ndiyo chanzo cha kukithiri kwa rushwa katika vyama vya siasa na Serikalini.

Dar es Salaam. Kutokuwepo kwa maadili katika ngazi ya jamii kumetajwa kuwa chanzo cha rushwa kwenye vyama vya siasa, ambapo ili mtu apate madaraka analazimika kutoa rushwa.


Hayo yameelezwa leo Novemba 30, 2022 na Mhariri wa Siasa Siasa wa Mwananchi, Salehe Mohamed wakati wa mjadala ulioandaliwa na kampumi ya Mwananchi Communications Ltd, kupitia Twitter Space, ukiwa na mada ikiwa ni ‘Kukithiri kwa rushwa kwenye chaguzi za vyama vya siasa, nini kifanyike?’


Amesema kwa Tanzania ukiangalia rushwa ilianza wakati wa mfumo wa vyama vingi tangu mwaka 1995 wakati uchaguzi huo uipofanyika kwa mara ya kwanza.


“Athari yake ni kubwa, kwani ili kiongozi apate nafasi fulani lazima awe na fedha, watu wasipokuwa na fedha hawezi kuchaguliwa.
Amesema Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kusema kitu ambacho ni hatari kwenye taifa ni rushwa, rushwa isipodhibitiwa inaweza kuwa hatari kwenye familia.