Usafirishaji binadamu unavyoleta msongo wa mawazo

Muktasari:
- Mwanasaikolojia Saldin Kimangale amesema tatizo la usafirishaji wa bianadamu linaleta madhara ya kisaikolojia hasa msongo wa mawazo.
Dar es Salaam. Mwanasaikolojia Saldin Kimangale amesema tatizo la usafirishaji wa bianadamu linasababisha madhara ya kisaikolojia hasa msongo wa mawazo.
Ameyasema hay oleo Desemba 6, 2022 katika mdahalo uliondeshwa kupitia Twitter ya Mwananchi (Mwananchi Twitter Space) ikiwa na mada ya ‘Usafirishaji haramu wa binadamu unavyochangiza ukatili nini kifanyike?’
Mwanasaikolojia huyo amesema japo hakuna takwimu za kuonyesha ukubwa wa tatizo hilo lakini suala la mtu kwenda eneo lingine na kuwekwa mateka humwathiri kisaikolojia.
Amesema inawezekana kusiwe na magonjwa ya moja kwa moja lakini tatizo la msongo wa mawazo kwa mhusika ni kubwa zaidi.
“Waanasaikolojia huwa tunajiuliza kwa nini watu wanafanya mambo ambayo kwao ni hatari? Ukweli ni kwamba anayeondoka anaathirika kisaikolojia iwe anayeachwa nyumbani yaani mzazi au mtoto wote wanapitia athari za kisaikolojia,” amesema.
Ili kukomesha tatizo hilo, Kimangale ameshauri wazazi kurejea kwenye majukumu yao ya kuwalea watoto kukabiliana na changamoto mbalimbali za kisaikolojia chini ya uangalizi wao.
Kwa upande wake Robert Mwaura amesema ili kumaliza tatizo hili ni muhimu kuwapatia watoto elimu ya kukabiliana na umasikini.
“Watoto wapewe elimu, unakuta mtoto, tukitaka kusaidia watu wa kwasababu watu wanatembea ni muhimu kuwapa mbinu sahihi ya kuishi katika mazingira tofauti,” amesema.