Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ukiwekeza maeneo haya ya kilimo hutojuta

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe. Picha na Baraka Loshilaa

Muktasari:


Wizara ya Kilimo imetaja baadhi ya maeneo ambayo wawekezaji ndani na nje ya nchi wanaweza kufaidika kwa urahisi.

Dar es Salaam. Kama unaishi Tanzania au nje na unataka kuwekeza kwenye kilimo na hujui uwekeze eneo gani, basi Wizara ya Kilimo  imeainisha maeneo muhimu ya kuwekeza.

 Baadhi ya maeneo ambayo kila mwekezaji anaweza kupiga dili, ni uzalishaji wa mbolea za kilimo, mbegu za kilimo, viuatilifu vya mazao, kilimo cha ngano, mafuta ya kupikia, parachichi, kuzisha vifungashio na kuongezaji thamani ya zao la korosho pamoja na kutengeneza vifungashio.

Maeneo hayo yenye fursa kwa wawekezaji wa kilimo, yametajwa na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe leo Jumatatu Desemba 18, 2023 wakati akizungumza na wawekezaji wa ndani kwenye kilimo jijini Dar es Salaam.

Bashe amesema kwa sasa asilimia 72 ya wakulima nchini ni wale wanaotumia ardhi ya ekari 2.5 na  asilimia 28 ndio wanaotumia ardhi kuanzia ekari 50 na kuendelea, hivyo lazima uwekezaji uongezwe walau kuwa ana asilimia 50 ya wakulima wenye ardhi kubwa.

"Malengo yetu ni kuongeza uzalishaji tuwe na kazi zenye hadhi nzuri kwa vijana kwenye sekta ya kilimo, tunataka kufikia 2030 tupunguze uingizaji wa mafuta kutoka asilimia 60 hadi 30,tunataka mkulima atoke kutumia mbolea kilogramu 19 hadi kilogramu 50,"amesema.

Kwa eneo la uzalishaji wa parachichi, Bashe amesema kilimo hicho kimeifanya Tanzania kushika nafasi ya tatu kwa uzalishaji Afrika lakini changamoto  ni matunda hayo kuharibika.

Dawa aliyoitaja kwenye eneo hilo, ni kuwaita wawekezaji wa viwanda vya uchakataji wa Parachichi kuwezesha parachichi hizo kuzalisha mafuta.

"Tunapoteza parachichi nyingi kwa kutofaa kuwa tunda mezani lakini inafaa kwa mafuta,"amesema.

Eneo la mbolea, Bashe ameeleza Serikali inafanya utafiti wa afya ya udogo nchini akisitiza kuwa uzalishaji wa mbolea nchini ni takribani tani 43,000 malengo ni kuwa na uzalishaji wa tani 1,000,000,

"Uzalishaji wa mbegu  mpaka sasa ni tani 49,880 malengo yetu ni  kufikia tani 652,250, pia uagizaji wa vifaa vya kilimo kutoka nje ya nchini tumeingiza trekta  6,190 na pawatila 6,409 kutoka nje ya nchi hili ni eneo la kuwekeza,"amesema.

Kwa upande wa maghala ya kuhifadhia chakula,Bashe amesema ni eneo muhimu ambalo sekta binafsi inapaswa kuwekeza kwani Serikali inakusudia kuhifadhi chakula tani milioni tatu.

Maeneo yenye uhitaji wa maghala hayo, Bashe amesema sekta binafsi ina nafasi ya kujenga maghala na kuikodishia Serikali na maeneo ya kujenga  yatatangazwa.

Eneo la vifungashio nalo ni changamoto, Bashe amesema kiwango kikubwa cha vifunganishio vinaingizwa kutoka nje ya nchi.

"Pia tunahitaji ujenzi wa viwanda vya korosho kuongeza thamani na ujenzi wa viwanda vya Mawese  katika mikoa ya Kigoma na Katavi,"ameeleza.

Kuhusu maeneo ya uwekezaji, Bashe amesema ekari milioni 44 za ardhi nchini zinafaa kwa kilimo na ekari milioni 15 pekee ndio zimetumika,

"Kwa eneo la umwagiliaji, ekari milioni 29 zilizopo nchini ni ekari milioni 0.82 ndio zimetumika,"ameeleza.

Bashe amehitimisha kwa kusema, miaka mitatu ijayo Sukari inayozalishwa Tanzania itatosha mahitaji ya ndani na itauzwa nje ya nchi.

Amesema uzalishaji wa sukari ni eneo ambalo halitahitaji uwekezaji kwani kutakuwa na utoshelevu wa sukari.


Baadhi ya wa wawekezaji wameiomba Serikali kuboresha uwezashaji wa wawekezaji na tatizo la mazao ya kurosho kushindwa kuongezewa thamani litakwisha.


Wanachosema wadau

Mmoja wa wawekezaji hao aliyejitambulisha kwa jina la Ismael Mohamed kutoka Usangu Logistics amesema changamoto ambaye Serikali inapaswa kuifungulia macho ni upatikanji wa ardhi kwa wawekezaji.

Amesema kwa muda mrefu ndani ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) amekuwa akifuatilia ardhi ili waanze kilimo lakini upatikanaji ni mgumu.

Changamoto hiyo inafanana na ya Morris Awil kutoka Kampuni ya Spice Limited ya mkoani Morogoro ambaye kwa muda mrefu amefuatilia ardhi bila majibu.

Naye Neva Mwambila wa Kampuni ya Plant difender ya mkoani Kilimanjaro amesema eneo la upotevu wa mazao shambani kutokana na wadudu Serikali iangalie kwa upekee.

Akielezea mkakati wa kuwawezesha wawekezaji hao,Waziri wa Mipango na  Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo amesema lengo la Serikali kuzifuta baadhi ya Taasisi zake na kuyaunganisha mashirika mengine ni kupunguza taasisi nyingi kudhibiti badala ya kuwezesha.

"Tasisi hizo zilianzishwa wakati Serikali ikitawala uchumi,nusu ya mashirika hayo zinashughulikia biashara zetu hiyo haiwezekani,mashirika mengi yatauawa lengo kutengeneza mazingira ya mazuri ya biashara,"amesema.