Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Uhakiki wafanyabiashara soko Kariakoo kuendelea wiki ijayo

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila akizungumza na wafanyabiashara katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa.

Muktasari:

  • Soko la Kariakoo liliungua Julai 2021, ili kufanya ukarabati wafanyabiashara hao walihamishiwa masoko ya Kisutu na Machinga Complex na sasa baada kukamilika linatarajiwa kuanza kazi tena mwezi ujao.


Dar es Salaam. Malalamiko ya wafanyabiashara waliokatwa kurudi soko la Kariakoo yamesikilizwa na sasa imeamuliwa kuwa shughuli ya kuhakikiwa kwa waliokatwa  majina yao itaendelea wiki ijayo siku ya Jumatatu.

Hatua hiyo imefikiwa leo Ijumaa Julai 12, 2014  kwenye mkutano kati ya wafanyabiashara hao na Mkuu wa Mkoa, Albert Chalamila, kusikiliza malalamiko yao baada kuandamana kwenda ofisi za CCM wakilalamikia wafanyabiashara zaidi ya 800 kuachwa katika orodha ya wanaotakiwa kurudi.

Juzi, Shirika la Masoko Kariakoo lilitoa orodha yake likionyesha  kati ya wafanyabiashara 1,861, wafanyabiashara 819 tu ndio wameonekana kukidhi vigezo vya kurudi hali iliyozua taharuki kwao na kufa ya maandamano jana ya kudai kurejeshwa wote.

Hata hivyo uhakiki huo utafanyika wakati ambao kuna manung’uniko kwamba majina yaliyotoka ya wanaopaswa kurejea soko la Kariakoo wapo wanaomiliki maduka zaidi ya matano.

Hadija Shomari mmoja wa wafanyabiashara, amesema maamuzi hayo anaamini yatatenda haki, kwani hata yeye pamoja na kuwa kiongozi wa eneo lake lakini jina lake lilikatwa.

Sheila Mfinanga amesema suala la kuongezwa gharama ya tozo  sio tatizo kwao, kwani  kikubwa ilikuwa ni kupata kwanza eneo kwa kuwa watakuwa tayari hata kwenda kukopa ilimradi wana uhakika wa kufanya biashara.


Maamuzi ya Chalamila

Chalamila katika maamuzi hayo, amesema viongozi hao wa jumuiya ya wafanyabiashara wakae pamoja na uongozi wa soko kujua namna gani watafanya shughuli hiyo, huku wakijua kuwa soko linatakiwa kufunguliwa mwezi ujao na Rais Samia Suluhu Hassan.

"Hivyo niwaombe katika uhakiki huu tunaoenda kuufanya tena hapa kuna timu ya kutoka Takukuru, Usalama wa Taifa, Jeshi la Polisi na za uchunguzi mwingine ambavyo ni vyombo vya serikali. Hivyo kwa mtu atakayethubutu kuleta janjajanja, niwaambie kila mtu atabeba msalaba wake," amesema Chalamila.

Hata hivyo Mkuu huyo wa Mkoa amewataka pamoja na kufanyika kwa uhakiki huo, wafanyabiashara hao kujua kwamba tozo walizokuwa wakilipa awali sizo watakazolipa kwa sasa watakaporejea sokoni kutokana na soko hilo kuboreshwa.

Wakitoa maoni yao kwa nyakati tofauti kuhusu uamuzi huo, wafanyabiashara hao walisema kushirikishwa kwa viongozi wao ndio walichokuwa wanakitaka tangu mwanzo lakini kwa bahati mbaya walipuuzwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa soko Dogo, Minja Msuya, amesema ushirikiano huo ungefanywa tangu mwanzo changamoto zilizotokea zisingekuwepo.

Kuhusu ni muda gani wanaweza kumaliza kuhakikiana, Msuya, amesema haitachukua hata siku tatu kwa kuwa wanajuana wote na kueleza muda wa kufunguliwa soko mwezi ujao wanaamini hautaathiriwa na shughuli hiyo ya uhakiki.