Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tume ya Haki za Binadamu walaani kutekwa Polepole

Dar es Salaam. Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), imelaani tukio la kutekwa kwa aliyekuwa  Balozi wa Tanzania nchini Cuba Humphrey Polepole.

Polepole aliyewahi kuwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ametekwa usiku wa kuamkia Oktoba 6, 2025 kwenye makazi yake Ununio jijini Dar es Salaam.

Jeshi la Polisi kupitia Msemaji wake, David Misime tayari limesema limeanza uchunguzi dhidi ya tukio hilo kubaini ukweli wake.

Kupitia taarifa iliyotolewa leo Oktoba 10, 2025 na tume hiyo na kusainiwa na Mwenyekiti wake Jaji mstaafu Mathew Maimu amesema tukio linalodaiwa kutendwa na watu wasiojulikana limeketa taharuki kwenye jamii.

"THBUB inalaani na kukemea vikali vitendo hivyo kwani matukio kama haya ni uvunjwaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa

misingi ya utawala bora ambayo yanahatarisha amani na utulivu

wa nchi yetu," amesema Jaji huyo kupitia taarifa yake.

Ikumbukwe tangu Polepole alijiuzulu nafasi yake Julai 13, 2025 na amekuwa akiibua tuhuma mbalimbali.

Miongoni mwa tuhuma hizo ni kuunganishwa kwa mifumo ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na Chama cha Mapinduzi (CCM) tuhuma ambazo Serikali ilieleza kuwa ni upotoshaji.

Pamoja na tuhuma hizo na zingine, Septemba 15, 2025 Jeshi la Polisi kupitia msemaji wake, David Misime lilieleza kuwa limefungua jalada la uchunguzi kuhusu tuhuma zilizotolewa  na Polepole.

Kutokana na tuhuma hizo, Jeshi la Polisi lilimtaka Polepole kufika  Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kutoa maelezo na ushahidi wa tuhuma alizoibua mtandaoni.

Hata hivyo, Polepole yeye alisema ipo nia njema na ovu kwenye wito huo hivyo akahoji kwa nini wasimhoji kwa njia ya mtandao.

"Kuna watu wanataka niende pale Polisi ukifika pale unakamatwa, kwa sababu hakuna sehemu wamesema kuna tuhuma kwangu, unaweza ukaachiwa halafu baadaye unapotea na Polisi hawahusiki," alisema Polepole Septemba 18, 2025 alipozungumza kwa njia ya mtandao akijibu wito wa polisi.