Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TRA wakamata Katoni 666 za pombe zenye stempu feki

Baadhi ya bidhaa zilizokamatwa katika kiwanda Cha Double Diamond Holdings zikiwa na stempu ambazo sio halali.

Muktasari:

  • Imebainija kuwa katoni zingine karibu 900 ambazo zimezalishwa muda mrefu lakini hazijabandikwa stampu kitu ambacho ni kinyume na sheria.

Arusha. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Arusha katika ukaguzi wake, wamebaini katoni 666 za pombe kali aina ya Double Diamond ambazo zimebandikwa stampu zinazodhaniwa ni za kughushi.

Aidha imebaini katoni zingine karibu 900 ambazo zimezalishwa muda mrefu lakini hazijabandikwa stampu kitu ambacho ni kinyume na sheria.

Akizungumza Mwananchi jana Oktoba 5, 2023, Meneja wa TRA Arusha Evaline Raphael amesema katika ukaguzi wa kuwatembelea wazalishaji wa bidhaa zinazobandikwa stempu za ushuru, ambapo timu maalum ya ukaguzi ilibaini stempu hizo.

"Timu imekuja kwa ajili ya kufanya ukaguzi wa kawaida tu na wamekutana na taarifa ambazo si sahihi.

"Katika kukagua uzalishaji wa kampuni hii ambayo inazalisha pombe kali aina ya Double Diamond,waligundua kulikuwa na katoni zaidi ya 600 ambazo zimebandikwa stampu zinazodhaniwa ni za kughushi," amesema

Amesema wakati wakiendelea na ukaguzi huo pia walibaini kwamba kulikuwa na katoni zingine karibia 900 ambazo zimezalishwa muda mrefu lakini hazijabandikwa stempu jambo ambalo ni kinyume na sheria.

"Wakati unapozalisha bidhaa inapotoka hatua moja kwenda nyingine lazima iwe imebandikwa stempu na mwisho iwe imehuishwa, tumekuta wakiwa na roller moja ambayo ni stempu zinazodhaniwa ni za kughushi," amesisitiza

Meneja huyo alitoa rai kwa wananchi kutumia app ya hakiki stamp wakati wowote wanapotumia bidhaa  kuzihakiki.

"Wazalishaji wengine tunatoa rai wasifanye hii ni michezo, ni hatari kwa sababu unahujumu uchumi wa nchi," ameongeza.

Hata hivyo, hakuna ofisa wa kiwanda cha Double Diamond Holdings aliyekuwa tayari kuelezea kuhusiana na stempu hizo.

Mwenyekiti wa chama Cha wafanyabiashara wenye viwanda na Kilimo (TCCIA) Mkoa Arusha, Walter Maenda akizungumza na Mwananchi ametaka wafanyabiashara kuacha kukwepa kodi na kama Kuna changamoto kufike katika Ofisi Cha TCCIA kupata ushauri.

Maenda amesema TCCIA tayari imeweke mazingira mazuri ya majadiliano ya kulipa Kodi mkoani Arusha hivyo hakuna sababu ya kukwepa kulipa Kodi

Naye Mkuu wa wa wilaya ya Arusha, Felishian Mtahengerwa akizungumza katika maadhimisho ya siku ya walipa Kodi Arusha aliwataka wafanyabiashara wa mkoa huo kuona suala la kulipa Kodi ni wajibu wa Kila mfanyabiashara.

 Mtahengerwa amesema kumekuwepo na tabia ya baadhi ya wafanyabiashara kukwepa Kodi au kwenda kwa baadhi ya viongozi kuwahonga wasilipe kodi jambo ambalo haliwasaidii.

"Hakuna kiongozi ambaye atakufutia deni TRA utampa pesa akusaidie atakula na hawezi na bahati mbaya fedha ambazo unatoa ungeweza kulipa Kodi na kutodaiwa," amesema.