Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TMA yatahadharisha hali mbaya ya hewa siku tano mfululizo, mvua

Muktasari:

  • Kesho Alhamisi, angalizo la mvua kubwa kwa maeneo machache ya mikoa ya Dar es Salaam na Pwani ikijumuisha visiwa vya Mafia, pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetangaza hali mbaya ya hewa kwa siku tano mfululizo katika mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Dar es Salaam, Kagera, Simiyu, Mara, Shinyanga na Mwanza.

Utabiri huo unaoanza leo Jumatano, Mei 7, 2025 umetolewa na TMA ukitoa angalizo la mvua kubwa na upepo mkali kwenye mikoa unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita 2.

Kuanzia leo Jumatano, TMA imebainisha mikoa ambayo inaweza kukutana na mvua kubwa ni Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara.

“Angalizo la upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita 2 limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wote wa pwani ya bahari ya Hindi (Mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Lindi na Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba),” imeeleza TMA.

Mamlaka hiyo imesema athari zinazoweza kujitokeza ni baadhi ya makazi kuzungukwa na maji, pamoja na kuathirika kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi, uvuvi na usafirishaji baharini.

Kesho Alhamisi, angalizo la mvua kubwa kwa maeneo machache ya mikoa ya Dar es Salaam na Pwani ikijumuisha visiwa vya Mafia, pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

TMA imetoa angalizo la upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita 2 limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wote wa pwani ya bahari ya Hindi (mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Lindi.

Ijumaa ya Mei 9, 2025, TMA angalizo la mvua kubwa limetolewa kwa maeneo machache ya mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Lindi na Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Jumamosi ya Mei 10, 2025 TMA imesema kutakuwa na mvua kubwa kwa maeneo machache ya mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Lindi na Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Jumapili ya Mei 11, 2025 hakutakuwa na mvua wala upepo.