Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Temesa yapata bosi mpya

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa),  Kheri Abdul Mahimbali. Picha na Mtandao

Muktasari:

  • Kheri amewahi kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Madini na baadaye akawa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati.

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amemteua Kheri Abdul Mahimbali, kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa).

Uteuzi wa Kheri unakuja miezi mitano tangu aliyekuwa na wadhifa huo, Lazaro Kilahala, asimamishwe kazi pamoja na watumishi wengine wa wakala huo.

Kilahala na wenzake walisimamishwa kazi Desemba 8, 2025 na Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, kupisha uchunguzi wa tuhuma za uzembe, usimamizi dhaifu na ubadhirifu.

Hatua ya kusimamishwa kwao, ilitokana na uchunguzi maalumu uliofanywa ndani ya Temesa na kubainisha ubadhirifu wa Sh2.5 bilioni.

Taarifa ya uteuzi wa Kheri, imetolewa leo, Jumapili Mei 3, 2026 na kutiwa saini na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bakari Machumu.

Kheri, amewahi kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Madini na baadaye akawa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati