Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Teknolojia kuondoa ubambikizaji bili za maji

Muktasari:

  • Matumizi ya teknlojia katika utendaji kazi ndani ya sekta ya maji umetajwa kuwa na manufaa ikiwemo kuondoa ubambikizaji wa bila za maji kwa wateja.

Dar es Salaam. Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema Serikali imejipanga kutumia teknolojia na hivyo kufanya mageuzi katika sekta ya maji, ambayo pia inaweza kuondoa changamoto ya mlaji kubambikiwa bili za maji.

“Haiwezekani suala la kubambikiza bili za maji liwe tatizo sugu ambalo limekosa mwarobaini, wenzetu wa India wako vizuri katika suala la teknolojia na tuko tayari kushirikiana kutafuta wadau ambao watawekeza katika kulipia maji kabla huduma (pre-paid),”

Aweso amesema lengo la kufanya hivyo ni kumfanya mwananchi kulipia kile alichotumia kama ilivyokuwa kwa umeme, kama amenunua wa Sh10, 000 basi atatumia nishati hiyo kwa kwa kiwango cha gharama ile aliyolipia.

Mageuzi mengine ambayo kama wizara imepanga kufanya ni kuwapo kwa teknolojia inayoweza kuonyesha sehemu ambayo maji yanavuja na hivyo kuiwezesha timu ya wataalamu kufika eneo husika na kulifanyia kazi katika muda muafaka.

Ametoa kauli hiyo leo wakati Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Zuhura Yusus alipokuwa akifanya mkutanao na waandishi wa habari juu ya mafanikio ya ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan nchini India.

“Mwananchi wakati mwingine anaweza kutuma ujumbe mfupi kuwa eneo fulani maji yanavuja lakini muitikio kutoka mamlaka ya maji husika ukawa ni mdogo sana, unaweza waziri ukatoa maelekezo wakayafanya lakini kwa sasa inabidi twende kidogo na teknolojia kwamba sehemu fulani pana vuja na timu ikafika kuchukua hatua,” amesema Aweso.

Amesema si busara kuona maeneo mengine maji yanapotea kwa kuvuja na kuna baadhi ya wananchi wanahangaika kupata huduma hiyo.

Akizungumzia mchango wa India katika utekelezaji wa miradi ya maji nchini, mbali na mradi wa zaidi ya Sh2 trilioni ambao utakwenda kutekelezwa sasa kutoka Ziwa Victoria, pia Sh356 bilioni ziliwahi kutolewa kwa ajili ya mradi wa maji Ruvu Juu kwenda Dar es Salaam na kujenga mradi wa Chalinze.

Mradi wa kutoa maji Ziwa Victoria unatarajiwa kutekelezwa kufuatia Tanzania kuwasilisha mahitaji yake katika benki ya Exim nchini India, kwa ajili ya mradi mkubwa wa umwagiliaji katika ziwa hilo, utakaogharimu Dola 1 bilioni za Kimarekani (Zaidi ya Sh2.505 trilioni).

Pia imeelezwa kuwa kutekelezwa kwa mradi huo utafaidisha mikoa ya Mwanza, Simiyu, Shinyanga, Singida, Dodoma, Kagera na Mara

“Pia kuna mradi wa Ziwa Victoria kwenda Tabora, Igunga, Nzega wa zaidi ya Sh617 bilioni ambapo zaidi ya vijiji 100 na watu zaidi ya milioni 1 wananuifaika na mradi huo,” amesema Aweso.

Katika hilo pia amesema wanaendelea kutekeleza mradi wa kimkakati wa zaidi ya Sh1.254 trilioni utakwenda kunufaisha miji 28 yenye shida ya maji na tayari wakandarasi wako kazini huku wananchi milioni 6 wakitarajiwa kunufaika.

Kuhusu Dodoma ambayo nayo itakuwa miongoni mwa wanufaika wa mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria, Aweso amesema lengo ni kuondoa tatizo la maji lililojitokeza baada ya Serikali kuhamia huko.

“Kabla Serikali kuhamia Dodoma, mahitaji ya maji yalikuwa milioni 44 lita na mamlaka yao ya maji ilikuwa na uwezo wa kuzalisha lita milioni 61, kwa sasa mahitaji ni lita milioni 140 hivyo tunapambana kuondoa tatizo hilo,” amesema.