Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TBS yazungumzia muda wa matumizi ya matairi

Muktasari:

  • Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limepiga marufuku matumizi ya matairi ya magari, pikipiki na baiskeli yanayotumika  zaidi ya miaka nane tangu yalipotengenezwa.


Dar es Salaam. Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limepiga marufuku matumizi ya matairi ya magari, pikipiki na baiskeli yanayotumika  zaidi ya miaka nane tangu yalipotengenezwa.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumamosi Oktoba 30,2021 jijini Dar es Salaam na ofisa viwango wa shirika hiyo, Arnold Mato wakati akitoa mada kuhusu viwango vinavyotakiwa kwa usalama barabarani katika semina ya waandishi wa habari iliyoandaliwa na Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA).

Amesema tairi la gari, pikipiki na baiskeli haliwezi kudumu kwa zaidi ya miaka nane na hiyo ni kwa sababu matairi huisha muda wake wa matumizi.

"Hivyo tafiti zinaonyesha tairi haliwezi kudumu kwa zaidi ya miaka 10 tangu lilipotengenezwa kiwandani, kwani mpira unaotumika kutengeneza tairi huisha  nguvu ikishapita miaka hiyo na matokeo yake upasuka.

"Ndio maana tunasema ili kuepuka  kupasuka kwa tairi wakati unaendesha chombo cha moto,  epuka kutumia kwa zaidi ya miaka hiyo niliyosema, badilisha kila wakati matairi ya gari lako ili liwe imara zaidi na lisiweze kukusababishia ajali," amesema

Naye mhandisi  wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (Tarura), Lutufyo Mwakigonja amesema baadhi ya barabara zinazotakiwa  kufanyiwa marekebisho huchelewa kukamilika   kutokana na fedha kutotosha.

“Tumekuwa tukipokea simu kutoka kwa wananchi juu ya kurekebisha barabara, tukienda na kukuta marekebisho yanataka fedha kidogo tunafanya lakini yakiwa makubwa hatuwezi kuyafanya kutokana na bajeti,” amesema.