Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tasac kuongeza nguvu kudhibiti uharamia wa meli

Muktasari:

  • Wakati jitihada za kudhibiti uharamia wa meli zikiendelea kufanywa nchini, matukio ya uharamia wa meli yanayoripotiwa duniani yameendelea kupungua hadi kufikia 116 mwaka 2024 kutoka 120 mwaka uliotangulia.

Dar es Salaam. Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (Tasac) limesema linaendelea kuimarisha mifumo yake ya ulinzi baharini kwa kutumia njia za kisasa ili kutokomeza uharamia wa meli zinazohudumiwa nchini.

Hilo linafanyika ili kuvutia watu wengi kutumia bandari za Tanzania ambazo zimeendelea kifanyiwa uwekezaji ili ziweze kuhudumia meli nyingi na zenye uwezo wa kushusha shehena kubwa ya mizigo.

Hayo yamesemwa leo Jumapili Julai 6, 2025 na Mwenyekiti wa Bodi ya Tasac, Mussa  Mandia wakati akizungumza na Mwananchi katika Maonyesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) maarufu Sabasaba yanayoendelea jijini hapa.

Amesema tofauti na miaka 10 hadi 15 iliyopita, matukio ya uharamia wa meli yaliyokuwa yakiripotiwa, sasa bahari ni shwari kutokana na jitihada mbalimbali wanazoendelea kufanya.

“Sasa tumejikita katika kuboresha usalama kwa kutumia vyombo vya kisasa ikiwamo satelaiti, drone pia kuna vituo mbalimbali vya ulinzi. Tunakusudia kuwa na vituo vingi zaidi kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama,” amesema.

Amesema kupitia yaliyofanyika sasa usalama uliopo baharini umefanya meli kuingia, kushusha na kupakia mizigo bila matatizo, biashara zinafanyika, ugunduzi wa gesi na mafuta unaendelea.

“Bahari ni salama kiasi cha kutokuwa na wasiwasi wa kufanya jambo lolote. Takwimu duniani kote zinaonesha kuwa asilimia 90 ya bidhaa zote husafirishwa kwa njia ya maji na Tanzania ikiwa ni miongoni mwa wasafirishaji kwani meli huingia kuleta mizigo na kupakia mizigo hivyo lazima tuimarishe usalama,” amesema.

Amesema mbali na kupambana na uharamia pia ni lazima wahakikishe meli zote zinazokuja nchini ni salama kwa ajili ya usafiri, usafirishaji na mazingira.

“Kwani bila kufanya hivyo, uchumi unaotokana na uvuvi utaathirika utalii wa fukwe utaathirika uvunaji mafuta na gesi bahatini utaathirika, hivyo pia tuko hapa Sabasaba kuwaonyesha wananchi namna tunavyoshiriki katika kulinda bahari ili nchi izidi kunufaika kiuchumi,” amesema.

Hili linasemwa wakati ambao matukio ya uharamia wa meli yanayoripotiwa duniani yameendelea kupungua hadi kufikia 116 mwaka 2024 kutoka 120 mwaka uliotangulia.

Taarifa hiyo kutoka Ofisi ya Kimataifa ya Masuala ya Baharini (IMB) kupitia kitengo maalumu cha Chama cha Kimataifa cha Biashara (ICC) inaonyesha kuwa meli 94 zilivamiwa moja kwa moja, kulikuwa na majaribio 15 ya uvamizi, meli sita zilitekwa nyara na meli tatu zilishambuliwa kwa risasi.

Ingawa idadi ya matukio yaliyoripotiwa mwaka 2024 inalingana kwa kiasi kikubwa na ya miaka miwili iliyopita.

Kupitia hilo, IMB ilitoa wito wa tahadhari zaidi ili kulinda usalama wa wafanyakazi wa meli kutokana na ongezeko la watu waliotekwa nyara au kushikiliwa mateka ambapo wafanyakazi 126 walitekwa mwaka 2024, ikilinganishwa na 73 mwaka 2023 na 41 mwaka 2022.

Pia, ripoti imeonesha ongezeko la matumizi ya silaha katika mashambulizi kwa kuwa, katika matukio 26 ya mwaka 2024, iliripotiwa kuwa silaha za moto zilitumika, ikilinganishwa na matukio 15 mwaka 2023.