Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanesco kusitisha huduma za kununua Luku kwa saa mbili

Muktasari:

Wateja wa huduma ya Luku kwa nchi nzima watakosa huduma hiyo kwa saa mawili kwa usiku wa Jumatano kuamkia Alhamis ya Juni 9 mwaka huu.

Dare es Salaam. Shirika la Umeme nchini (Tanesco) limesema wateja wa huduma ya ununuzi wa umeme kupitia Luku watakosa huduma hiyo kwa saa mbili kwa usiku wa Jumatano kuamkia Alhamisi Juni 9 mwaka huu.

Huduma hiyo itakosekana kuanzia saa 6 usiku hadi saa 8 usiku nchi nzima ili kupisha maboresho ya mfumo wa manunuzi ya umeme kwa wateja wanaolipia kabla ya matumizi (Luku), kupitia mifumo iliyopo katika kituo cha kujikinga na majanga (Disaster Recovery).

Akizungumza leo Juni 06/2022 kwenye makao makuu ya taasisi hiyo, Meneja Mwandamizi wa Tehama, Cliff Maregeli amesema kutokana na changamoto hiyo ya kiufundi wateja wanashauri kununua umeme wa ziada ili kuepuka usumbufu ambao unaweza kujitokeza.

"Maboresho ni muhimu na yanalenga kuongeza ufanisi kwenye mfumo wa manunuzi ya umeme ili kuhudumia wateja wengi ipasavyo pale inapotokea hitilafu ya aina yeyote katika kituo chetu Kikuu Cha mfumo," amesema Maregeli

Kwa uapande wake Msemaji wa Shirika hilo, Martini Mwambene ameshauri wateja kuzingatia taarifa hiyo ili kuruhusu maboresho hayo ya mfumo kufanyika.