Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Takukuru yawafikia watoto njiti Shinyanga

Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Crispin Francis Chalamila (kulia), akimkabidhi Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dk John Luzila, vifaa tiba kwa ajili ya watoto njiti vilivyotolewa na watumishi wa Takukuru.

Muktasari:

  • Vifaa vilivyotolewa ni mashine ya kutoa joto kwa watoto wachanga na mashine ya kutibu ugonjwa wa manjano kwa watoto wachanga, ambavyo vimenunuliwa kupitia michango ya hiari ya watumishi wa Takukuru nchini.

Shinyanga. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imekabidhi vifaatiba vya kisasa kwa ajili ya kuwahudumia watoto waliozaliwa kabla ya wakati, njiti katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto.

Akizungumza leo Juni 3, 2026 wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Mkurugenzi mkuu wa Takukuru, Crispin Chalamila ameeleza kuwa, hatua hiyo ni sehemu ya mchango wa watumishi wa Takukuru katika kuunga mkono jitihada za Serikali za kuimarisha huduma za afya nchini.

“Tumeamua kuunga mkono jitihada hizi kwa kununua vifaatiba kwa ajili ya hospitali mbalimbali nchini, tayari tumetoa vifaa hivi katika mikoa 19 na Shinyanga ni mkoa wa 20 lengo letu ni kufikia mikoa yote 28 ya Tanzania bara, vifaa hivi vimenunuliwa kupitia michango ya hiari ya watumishi wa Takukuru,” amesema Chalamila.

Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Crispin Francis Chalamila akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa tiba vilivyotolewa na watumishi wa Takukuru kwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Chalamila ametoa wito kwa taasisi, mashirika na wananchi wengine kuendelea kushirikiana na serikali katika kuboresha huduma za afya, akisisitiza kuwa mahitaji ya vifaatiba katika hospitali bado ni makubwa.

“Serikali haiwezi kufanya kila kitu peke yake, tunawaomba wadau wengine wajitokeze na kuunga mkono juhudi hizi kwa kutoa michango yao ili kusaidia kuboresha huduma za afya, hususan kwa mama na mtoto” ameongeza.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dk John Luzila ameishukuru Takukuru kwa msaada huo akieleza kuwa vifaa hivyo vitasaidia kuongeza uwezo wa hospitali katika kuwahudumia watoto njiti na wenye uzito mdogo wanaohitaji uangalizi maalum,

Amesema kuwa, msaada huo wa Takukuru unatarajiwa kuongeza uwezo wa hospitali hiyo kutoa huduma bora kwa watoto wachanga, hususan njiti hivyo kuchangia kupunguza vifo vya watoto pamoja na kuboresha afya ya mama na mtoto katika mkoa wa Shinyanga.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dk John Luzila akizungumza wakati wa hafla ya kupokea vifaa tiba kwa ajili ya watoto wachanga vilivyotolewa na watumishi wa Takukuru.

“Tunatoa shukrani za dhati kwa watumishi hawa kwa msaada huu mkubwa, haya ni matendo ya huruma yanayogusa maisha ya watoto wachanga, vifaa hivi vimekuja katika wakati muafaka na vitasaidia kuboresha huduma tunazotoa kwa watoto waliozaliwa kabla ya wakati,” amesema Dk Luzila.

Pia, ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuweka mazingira rafiki yanayowawezesha wadau mbalimbali kushiriki katika kuboresha huduma za afya, huku akitoa mwaliko kwa wadau wengine kujitokeza kusaidia sekta hiyo muhimu.