Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tafiri kufanya tafiti kuhusu mchango sekta ya uvuvi nchini

Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utafiti pamoja na Uratibu wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (Tafiri) Dk Mary Kishe akibainisha umuhimu wa tafiti mpya katika uvuvi jijini Dar es Salaam

Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (Tafiri), imesema inafanya tafiti ili kupata taarifa sahihi juu ya rasilimali za uvuvi zilizopo hapa nchini, lengo likiwa ni kuiwezesha sekta hiyo kuchangia zaidi katika pato la taifa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Oktoba 9, 2023 katika warsha ya watafiti wa uvuvi; Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uvuvi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Stephen Lukanga amesema katika kufanya tafiti hizo, Tafiri itashirikiana na Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) pamoja na Chuo Kikuu Cha DUKE cha nchini Marekani.

“Tafiti hizo zitaiwezesha Serikali kuweka taarifa zake sahihi kulingana na idadi ya watu ambao wamekuwa wakinufaika kupitia rasilimali zilizopo majini nchini Tanzania,” amesema Kaimu Mkurugenzi huyo na kuongeza;

“...Kwa sasa idadi ya watu nchini imeongezeka na kufikia zaidi ya milioni sitini, ila bado taarifa zilizopo kwenye sekta ya uvuvi zinatolewa kulingana na idadi ya watu iliyokuwepo zamani (takriban watu milioni 40), ambazo zimekuwa zikibainisha kuwa watu wanaojishughulisha moja kwa moja katika sekta ya uvuvi ni milioni 4.5.”

Aidha, amesema warsha hiyo imeanzishwa na wanasayansi na watafiti kutoka nchi zaidi ya 58 kuhakikisha rasilimali ambazo hazijionyeshi kwa uwazi, ziweze kuonekana hususan kwenye uvuvi mdogo ili kuongeza mchango wa sekta ya uvuvi katika pato la taifa.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utafiti pamoja na Uratibu wa Tafiri, Dk Mary Kishe, amesema taasisi hiyo ambayo mwaka huu inafikisha miaka 40, imekuwa ikikusanya na kutafiti masuala mbalimbali ya sekta ya uvuvi lakini bado haijaangalia mchango wa sekta hiyo kwenye pato la taifa na mtu mmoja mmoja.

Amesema kupitia warsha hiyo inayoendelea jijini Dar es Salaam, taasisi hioz tatu, zitaweza kuunganisha taarifa za zamani na kuziweka pamoja na kuona umuhimu wa takwimu hizo kwa maendeleo endelevu ya sekta ya uvuvi kwa kuwa kuna taarifa ambazo zimejificha ambazo hazionyeshi usahihi juu ya sekta hiyo.

Pia, amesema warsha hiyo ni muhimu ambapo watafiti watapata fursa ya kutoa mapendekezo yao ya namna ya kusimamia rasilimali za uvuvi ili kuweza kufikia lengo la sekta ya uvuvi kuongeza mchango zaidi katika pato la taifa.

Kwa upande mwingine, maofisa wawili kutoka fao ambao ni Ofisa Mkuu Nicolas Gutierrez na Ofisa Mipango Mtafiti, Nicole Franz kwa nyakati tofauti wamesema uwepo wa taarifa sahihi ni muhimu katika kuendeleza sekta ya uvuvi pamoja na kulinda rasilimali za uvuvi nchini.

Wamebainisha pia uwepo wa taarifa sahihi ya sekta ya uvuvi utawezesha kubadili maisha ya watu wanaojishughulisha na uvuvi hususan wavuvi wadogo kwa kuangalia namna wanavyochangia katika sekta hiyo kwa kuwa ni sekta ambayo inachangia katika ongezeko la chakula duniani.

Warsha hiyo ambayo ni muhimu katika kuangalia mchango wa sekta ya uvuvi nchini, inafanyika kwa siku tano jijini Dar es Salaam.