Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sifa kuu tatu Dira 2050, hatua nne zatajwa

Muktasari:

  • Dira 2050 ustawi wa pamoja ambapo inazinduliwa na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, imepitia hatua mbalimbali hadi kukamilika kwake. Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dk Fred Msemwa ameelezea safari ya kupatikana kwake.

Dodoma/Dar. Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dk Fred Msemwa ametaja sifa kuu tatu za Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025-2050, akisema kuwa dira hiyo ni shirikishi, inahusisha wataalamu wa Kitanzania na gharama zote za uandaaji wake zimetolewa na Serikali.

“Sifa ya kwanza ni shirikishi, ambapo makundi yote ya kijamii na watu binafsi walishirikishwa katika michakato yote. Sifa ya pili ni kuhusisha wataalamu wa Kitanzania katika hatua zote za maandalizi, uchambuzi, uandishi, na uhakiki wa dira hiyo.

Upekee wa tatu ni kwamba gharama zote za uandaaji wa Dira hiyo zimefadhiliwa na Serikali kupitia Wizara ya Fedha,” amesema Dk Msemwa.

Dk Msemwa ameyaema hayo leo Alhamisi Julai 17, 2025 wakati wa uzinduzi wa Dira hiyo katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma, ambapo mgeni rasmi ni Rais Samia Suluhu Hassan.

Katika mtendaji huyo amesema katika maandalizi ya Dira hiyo, hatua nne zilizochangia kukamilika ikiwamo kuwafikia Watanzania moja kwa moja kwenye kaya zao.

Amesema hadi dira hiyo inakamilika watu zaidi ya milioni 1.17 walifikiwa na kutoa maoni yao huku njia saba zilitumika ikiwamo utafiti katika ngazi ya kaya na watu zaidi 15,000 walifikiwa.

Njia nyingine zilizotumika ni kukusanya maoni kwa njia ya simu nchi nzima, wananchi walipigiwa na kuulizwa masuala tofauti, ujumbe kwa njia ya simu (USSD) watu 1.19 milioni walifikiwa na asilimia 82 wakiwa vijana chini ya miaka 36.

Pia, kupitia tovuti maalumu na Desemba mwaka jana watu 13,459 walitoa maoni, tulifanya makongamano 12, watu 22,779 walihudhuria, viongozi waliopo madarakani na wastaafu 44 walihojiwa kutoa maoni yao.

Amesema semina mbalimbali zilifanyika, kukusanya nyaraka 33 zinazoelezea historia ya maendeleo ya Tanzania na zilichambuliwa.

Mbali na kukusanya maoni pia walijifunza kutoka nchi zilizopiga hatua za kimaendeleo katika Bara la Afrika, Asia na Ulaya huku baadhi ya nchi walizojifunza ni Botswana, Moroco, Mauritius, Afrika Kusini na Kenya.

Mchakato rasmi wa maadalizi wa Dira 2050 ulizinduliwa Aprili 3, 2023 na Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango na baada ya kuzinduliwa mchakato wa kuunda vyombo vya kitaasisi vya kusimamia uandishi wa dira ulianza.

Dk Msemwa amesema baada ya rasimu kupatikana ilirudishwa kwa wadau ili kupata maoni ya kiuhariri, kukutana na wadau mbalimbali, waandishi, vyama vya siasa 19 ili kuhakikisha kunakuwa na sauti ya pamoja na baadaye walipitia maoni ya wadau yaliyotolewa na kuyafanyia kazi.

Machi 28, 2025, rasimu ya pili ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ilikabidhiwa kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na baadaye ikaingizwa serikalini.

Dira hiyo ilipitishwa na katika baraza la mawaziri Juni 22, 2025 kwa ajili ya kuidhinishwa kabla ya kuwasilishwa bungeni Juni 26, 2025 ambapo Bunge liliridhia rasmi ikiwa ni hatua ya kuiwekea ulinzi kwa azimio la Bunge.


Endelea kufuatilia Mwananchi