Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Shahidi kesi wizi Sh1.6 bilioni za benki akosekana mahakamani

Muktasari:

  • Kesi inayomkabili raia wa Ghana, Valentine Zacheus na mtanzania, Fortunatus Bundara imeshindwa kusikilizwa ushahidi kutokana shahidi aliyetegemewa ana matatizo ya kifamilia.

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu katika  kesi ya wizi wa Sh1.6 bilioni mali ya Benki ya ABC inayowakabili raia wa Ghana, Valentine Zacheus na Mtanzania, Fortunatus Bundara imeshindwa kusikilizwa ushahidi kwa kuwa shahidi aliyetarajiwa hajafika mahakamani.

Wakili wa Serikali, Winia Samsoni alidai hayo leo Oktoba 20, 2023 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Arodia Kyaruzi kuwa shahidi waliyemtarajia hajafika kwa kuwa ana matatizo ya kifamilia.

"Shauri hili lilikuja kwa ajili ya kusikiliza ushahidi lakini shahidi niliyemtegemea ana matatizo ya kifamilia," amedai Samson.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Kyaruzi aliahirisha shauri hilo hadi Novemba Mosi, 2023 kwa ajili ya usikilizwaji.

Katika kesi ya msingi inadaiwa washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kula njama ya kutenda kosa la wizi na wizi.

Inadaiwa kuwa katika tarehe tofauti kati ya Oktoba Mosi, 2021 na Julai 31, 2022, washtakiwa hao walikula njama ya kutenda kosa la wizi.

Alidaiwa kuwa washtakiwa hao walishirikiana na kufanikiwa kuingilia mfumo wa benki hiyo na kuiba Sh1.6 bilioni.