Serikali yatoa Sh900 milioni ujenzi wa daraja la Rau

Mbunge wa Moshi vijijini profesa Patrick Ndakidemi (aliyevalia shati jeupe) akipokea maelekezo ya ujenzi wa darala la Rau kutoka kwa Mhandisi Mnene James
Muktasari:
- Serikali yatoa zaidi Sh900 milioni kwa ajili ya ujenzi wa daraja la Rau lilosombwa na mafuriko yalisababishwa na mvua kubwa zilizonyesha mwaka jana.
Moshi. Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini, Profesa Patrick Ndekidemi amesema Serikali imetoa Sh900 milioni kwa ajili ya ujenzi wa daraja la Rau ambalo lilosombwa na mafuriko.
Daraja hilo ambalo lilisombwa na maji mwaka jana baada ya mvua kunwa kunyesha lilikuwa kiungo kati ya Kata ya Rua na Uru Mashariki.
Profesa Ndekidemi amesema hayo leo Julai 30, 2020 katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo katika jimbo lake ambapo amesema, kuvujika kwa daraja hilo kulipelekea kutenganisha wananchi wa kata za Rua na Uru Mashariki.
Amesema daraja hilo lilikwamisha miradi mingi ya Serikali kama ujenzi wa barabara ya Materuni na barabara ya Shimbwe ambapo daraja hilo lilikuwa likiunganisha maeneo hayo.
"Wananchi walishindwa kufanya shughuli za kijamii kama kusafirisha mazao kwa ajili ya biashara, kupata huduma za hospitali pamoja kupitisha maiti" amesema Ndakidemi.
Meneja wa Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini (TARURA), Mhandisi Mnene James amesema ujenzi wa daraja hilo utakamilika mwezi Oktoba mwaka huu.
Kukatika kwa daraja hilo kulileta adha kubwa kwa wananchi katika shughuli zao za kijamii na kiuchumi.