Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali yakaribisha Waarabu kuwekeza kwenye kilimo

Muktasari:

  • Wawekezaji hao kutoka nchini Oman wamekuja nchini kufuatia ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyoifanya katika nchi hiyo Juni mwaka huu.

Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe amewakaribisha wawekezaji kutoka Jumuiya ya nchi za Kiarabu kuja kuwekeza katika sekta za kilimo na mifugo, ili kukuza uhusiano wa kibiashara.

Ameyasema hayo juzi Julai 19, 2022 jijini hapa wakati Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kilipokuwa kikipokea ujumbe kutoka Jumuiya ya nchi za Kiarabu waliokuja kuangalia fursa za uwekezaji katika sekta ya kilimo na mifugo.

Akizungumza katika mkutano huo, Waziri Kigahe amesema Tanzania na Oman ni washirika wa muda mrefu hasa katika fursa mbalimbali za kibiashara.

“Hata hivyo, hatujatumia fursa hizo kikamilifu, ninaamini tunaweza kufanya vizuri zaidi kwa sasa na ninatoa wito kwa mamlaka za serikali katika nchi zote mbili kufanya kazi kwa pamoja ili kuruhusu mtiririko mzuri wa bidhaa na huduma kati ya nchi hizi mbili,” amesema Kigahe.

Amesema Tanzania inaungana na kuwa nchi yenye nguvu ya kilimo barani Afrika na miradi hii itaongeza kasi ya safari kuelekea mafanikio hayo.

“Hadi kufikia Juni 2022 jumla ya miradi 62 ya uwekezaji imesajiliwa nchini Tanzania na raia wa Oman, miradi hii inatarajiwa kutoa ajira 2,488 ikiwa na thamani ya Uwekezaji wa zaidi ya Dola za Marekani 308.35 milioni na sekta zinazoongoza katika idadi ya miradi ni viwanda na majengo ya biashara, uchukuzi na utalii na sekta zote hizi zinachangia zaidi pato la Taifa,” amesema.

Naye balozi wa Tanzania nchini Oman, Abdallah Kilima aliyeambatana na ujumbe huo amesema, ziara hiyo ni hatua za utekelezaji wa maombi yaliyojitokeza wakati wa ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan alipotembelea nchini Oman Juni 2022.

“Ujumbe huu umejumuisha wawakilishi kutoka taasisi za Oman Food Investment Holding Company ambao ndio waratibu wakubwa wa ziara hii na muwakilishi wake ni Mhandisi Saleh Al Shanfari ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu.

“Pia imejumuisha taasisi ya Arab Authority for Agriculture Investment and Agriculture Development ambayo imewakilishwa na Mohammed Mazrooei, Mwenyekiti na Rais wa Mamlaka husika ambaye pia ndie kiongozi wa ujumbe huu,” amesema Balozi Kilima.

Amezitaja pia Arab Bank for Economic Development in Africa iliyowakilishwa na Mkurugenzi Mkuu wake Dk Sidi Ould Tah pamoja na kampuni ya Al-Rajhi International for Investment kutoka Saudi Arabia, Mamlaka ya Uwekezaji nchini Oman (Oman Investment Authority-OIA) pamoja na kampuni ya nyama ya Al-Bashayer Meat  Co. SAOC.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Uhamasishaji Uwekezaji wa TIC, Revocatus Rasheli amesema,

wamepata waliojikita katika eneo la kilimo na ufugaji ikiwa ni mpango wa miaka mitano wa kuimarisha usalama wa chakula nchini.

“Katika majadiliano yanayoendelea TIC imeratibu na imeweza kuwaleta wadau mbalimbali wa taasisi za serikali na binafsi zinazohusika na uwekezaji na biashara katika sekta hizo za kilimo na uzalishaji wa mazao ya biashara pamoja na mifugo,” amesema Rasheli.