Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali yaja na suluhisho mafuriko Jangwani

Muktasari:

  1. Serikali imeweka mkandarasi maalumu katika eneo la jangwani ambaye anafanya kazi ya kusafisha mto huo mita 500 kila upande wakati wote wa mvua.

Dodoma. Serikali imeweka mkandarasi maalumu katika eneo la jangwani ambaye anafanya kazi ya kusafisha mto huo mita 500 kila upande wakati wote wa mvua.

Kwa hali hiyo, suala la usumbufu wakati wa msimu wa mvua ambao wananchi wamekuwa wakiupata na kuona eneo hilo ni kero kubwa.

Kauli ya Serikali imetolewa bungeni leo Juni 8, 2022 na Naibu Waziri wa Ujenzi, Godfrey Kasekenya ambaye amesema mradi wa ujenzi kwenye daraja hilo ni Julai 2022.

Naibu Waziri alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Asha Abdallah Juma ambaye amehoji ni lini Serikali itajenga daraja katika eneo la Jangwani Barabara ya Morogoro jijini Dar es Salaam ili kuondoa usumbufu na adha wanazopata wananchi hasa wakati wa mvua?

Naibu Waziri amesema Kazi ya Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina kwa ajili ya ujenzi wa Daraja jipya la Jangwani chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia ili kutatua tatizo la mafuriko imekamilika.

Kasekenya amesema Serikali inaendelea na mazungumzo na Benki ya Dunia ili kupata fedha kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo.

Hata hivyo, majibu hayo hayakumridhisha Mbunge wa Kinondoni Abbas Talimba ambaye ameomba mwongozo wa Spika akisema majibu ya ujenzi wa daraja hilo yamekuwa yakitofautiana mara kadhaa Serikali inapojibu swali hilo.

Talimba alisema awali waliambia kuwa ujenzi wa daraja hilo ungeanza Julai mwaka huu baada ya taratibu zote kukamilika kwenye ujenzi huo.

Spika wa Bunge amemtaka mbunge huyo kuomba mwongozo katika swali ambalo angekuwa ameuliza yeye lakini ya siku nyingi hanayo eneo hilo ka wakati huo na hiyo ikawa nafuu kwa Wizara ya Ujenzi.