Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali, wadau kusaidia hedhi kwa wanafunzi

Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais (Tamisemi), Angela Kairuki akiongoza mbio (Run for Binti Marathon) zilizoandaliwa na Shirika la Msaada wa kisheria (LSF) na Smile for Children (S4C) na kufanyika jijini hapa jana Julai 30, 2023

Muktasari:

  • Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais (Tamisemi), Angela Kairuki amesema pamoja na juhudi zinazofanywa na Serikali kujenga miundombinu ya shule, itashirikiana na wadau kuweka vifaa vya hedhi salama kuwawezesha wanafunzi wa kike kuhudhuria shule.

Dar es Salaam. Serikali imesema itashirikiana na wadau kuwezesha ujenzi wa miundombinu na kununua vifaa vya hedhi kwa wanafunzi wa kike ili kuwawezesha kupata elimu na kutimiza ndoto zao.

Hayo yameelezwa jana Julai 30 na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais (Tamisemi), Angela Kairuki baada ya kushiriki mbio (Run for Binti Marathon) zilizoandaliwa na Shirika la Msaada wa kisheria (LSF) na Smile for Children (S4C) na kufanyika jijini hapa.

Lengo la mbio hizo lilikuwa ni kukusanya fedha kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya hedhi ukinga kufaidisha watoto wa kike wapatao 15,000 katika mikoa ya Lindi na Mtwara na kusaidia vikundi vya wanawake kushona sodo na kuziuza kwa wanajamii.

Waziri Kairuki amesema pamoja na juhudi za Serikali za ujenzi wa shule za msingi na sekondari, bado kuna haja ya kuongeza huduma za hedhi kwa wasichana ili wahudhurie masomo ipasavyo.

“Tamisemi tumekuwa atukishirikiana na wadau mbalimbali katika sekta ya elimu kuhakikisha tunaimarisha miundombinu ya afya na elimu.

“Katika mkakati wa kuhakikisha hedhi salama, Serikali tumeboresha miundombinu hasa vyoo, tumeweka vyumba kwa ajili ya watoto wa kike kubadilisha sodo zao katika shule 1,283 na tunaendelea kufanya hivyo na lengo letu ifikapo mwaka 2025/26 tuwe tumefikia shule takriobani 2,500,” amesema.

Akieleza ukubwa wa tatizo la hedhi kwa maendeleo ya elimu ya watoto wa kike, Waziri Kariruki amesema, kwa mwezi watoto wa kike hukosa masomo kati ya siku tatu hadi, hali inayosababisha wasifanye vizuri katika mitihani na wengine huacha shule kabisa.

Ameipongeza LSF kwa kufadhili mbio hizo zinazolenga kujenga na kukuza ustawi wa mtoto wa kike katika nyanja mbalimbali ikiwemo elimu, kijamii na kiuchumi.

“Mapato yatakayopatikana katika mbio hizi yatawezesha watoto wa kike katika mikoa ya Lindi na Mtwara kupata vifaa vya hedhi salama na kuwalinda na magonjwa na vitawawezesha kuhudhuria shuleni na kuongeza ufaulu wao,” amesema.

Serikali kupitia kwa mheshjimiwa Rais Samia Suluhu Hassna imekuwa ikijenga shule nyingi na wadau wetu wamekuwa sehemu ya mafanikio.

Awali akizungumza, Mkurugenzi Mtendaji LSF, Lulu Ng’wanakilala amesema mbio hizo ni mwendelezo wa kazi za shirika hilo za kupigania upatikanaji wa haki kwa watu wote hasa wanawake na watoto wa kike.

“Tunazungumzia haki za uzazi, haki za uchumi, tunazungumzia haki za mtoto wa kike kushiriki katika elimu, mtoto wa kike kutoingizwa katika ukatili wa kijinsia.

“Fedha zitakazokusanywa zitalwenda kuwasaidia watoto wa kike ili waendelee na masomo,” amesema.

Naye Mkurugenzi wa S4C, Flora Njelekela amesema lengo la mikakati hiyo ni kumlinda mtoto wa kike na kumsaidia kufikia ndoto zake.

“Mtoto huyo wa kike anapitia changamoto nyingi anapokuwa kwenye hedhi, hivyo tukaona tukusanye fedha kwa ajili ya kununua bidhaa sahihi za hedhi zikiwemo za kutupa na kurudia ili zimsaidia mtoto huyu abaki shuleni,” amesema.