Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali kutoa huduma ya intaneti majumbani

Muktasari:

  • Naibu Waziri wa Habri na Mawasiliano, Mathew Kundo amesema Serikali imejisatiti kutoa huduma ya intaneti majumbani kupitia kampuni ya TTCL ili kuwarahisishia Watanzania wenye uhitaji wake.

Arusha. Serikali imeanza kusambaza huduma za intaneti kwa bei nafuu zaidi katika makazi ya watu ili kurahisha utendaji wa kazi ambazo zinahitaji huduma hiyo.

 Huduma hiyo, tayari imeanza kusambazwa katika majiji ya Dodoma na Dar es Salaam na inatarajiwa ifikapo mwaka 2027 zaidi ya nyumba milioni moja kuwa tayari zimefungwa intaneti.

Naibu Waziri Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mathew Kundo amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufungua kikao cha baraza la uongozi la Umoja wa Posta Afrika (PAPU) jijini Arusha leo Agosti 28, 2023.

Kundo amesema huduma hiyo inatolewa na kampuni ya simu ya TTCL na imepewa jina la Fiber to home.

Amesema kupitia huduma hiyo, nyumba ambazo zitahitaji huduma hiyo, zinapeleka maombi TTCL na baadae kufungiwa intaneti kupitia nguzo za umeme zilizokaribu na makazi yao na kuuunganishwa moja kwa moja na mkongo wa Taifa wa mawasiliano.

"Huduma kupitia mradi huu zitakuwa rahisi zaidi na zenye kasi, mimi binafsi tayari nyumbani kwangu Dodoma nimefungiwa huduma hii na imepunguza sana gharama za matumizi intaneti," amesema.

Amesema mradi huo, unatokana na utekelezwaji wa maagizo ya Rais Samia Suluhu, kuboresha huduma za mawasiliano nchini ambapo wanufaika wengine ambao watapata huduma hiyo ni shule, vituo vya mabasi na sehemu zenye mkusanyiko wa watu.

"Tunaelekea katika matumizi makubwa ya huduma za kidigitali nchini, ikiwepo kununua, kuuza bidhaa mbali mbali na hivyo haitakuwa lazima watu kutembea na fedha mikononi ama kuweka fedha majumbani," amesema.

Amesema matumizi hayo ya intaneti yatasaidia pia suala la anuani ya makazi na kupitia mfumo wa NAPA ambapo itakuwa rahisi kujua kila mtu alipo na hivyo kupelekewa huduma mbali mbali ambazo atahitaji.

"Kama mtu anakutumia bahasha ama mzigo utalelewa mpaka nyumbani, lakini pia kama unahitaji huduma kama za afya na nyingine kupitia mfumo wa NAPA utaonesha sehemu ambayo huduma hiyo ipo kwa urahisi zaidi," anasema.


Baadhi ya wakazi wa Arusha, wakizungumzia huduma hiyo na kupata intaneti majumbani walieleza itasaidia sana kupunguza gharama za maisha lakini pia kunufaika na huduma za mtandaoni.

Salma Ally ambaye ni mwanafunzi chuo cha Uhasibu Arusha, alisema kwa wanafunzi huduma hiyo itasaidia sana kujisomea na kupata vitabu mbali mbali vilivyopo mitandaoni.

"Tumekuwa tukilipa bando kubwa kufatilia masomo na kupakua vitabu lakini sasa huduma hii itarahisha sana kujiendeleza kielimu," alisema.

John Shirima mkazi wa Sakina aliomba Serikali kuharakisha mradi huo kwani bado kuna maeneo haujafika kama Arusha.

"Mimi tayari nilienda TTCL kuomba hii huduma ila wameniambia nisubiri hivi karibuni nitapata, naimani itasaidia hasa kwa sisi wafanyabiasha ambao tunatumia mitandao kufanyabisahara zetu," amesema.