Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali kufufua Shirika la Uvuvi, kuinua uchumi

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Jenista Mhagama (katikati) akipokea maelezo kutoka kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tafico Dennis Simba, alipotembelea ofisi za shirika hilo leo Alhamis ya Julai 27, 2023. Picha na Sute Kamwelwe.

Muktasari:

  • Serikali ya Tanzania ipo kwenye mchakato wa kulifufua shirika la uvuvi (TAFICO), ikiwa ni lengo la kuinua uchumi kupitia mazao bahari, sambamba na kuwawezesha wananchi kupata lishe bora inayopatikana kwenye samaki.

Dar es Salaam. Katika juhudi za kuinua uchumi wa nchi kupitia uvunaji wa mazao bahari, Serikali inaendelea na mchakato wa kulifufua Shirika la Uvuvi (Tafico), ambalo litaendesha shughuli za uvuvi wa samaki hadi uuzaji.

Serikali imesema kwa sasa inaendesha mradi wa ununuzi wa vifaa na miundombinu wezeshi ambapo shirika litafanya uvuvi katika bahari kuu kwa mara ya kwanza kwenye kina kirefu cha bahari.

Akizungumza leo Julai 27, 2023 alipotembelea ofisi za Tafico zilizopo Rasi ya Mkwavi iliyopo Kigamboni, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama amesema lengo la Serikali ni kuona fursa iliyopo baharini inatumika vyema.

Mhagama ambaye ametembelea ofisi hizo za Tafico ikiwa ni jukumu la kiuratibu la Wizara yake amesema Serikali inahakikisha inaongeza tija na faida katika mazao yatokanayo na bahari.

"Kupitia mradi huu Serikali itatengeneza meli kubwa nne za uvuvi, itajenga kiwanda cha samaki Kilwa pamoja na kuwajengea uwezo mabaharia kwenye uvuvi wa bahari kuu kwa kuwapa mafunzo sambamba na kugharamia uendeshaji wa meli hizo," amesema Mhagama.

Aidha amesema Serikali itajenga kiwanda cha barafu pamoja na kununua magari mawili malumu ya ubaridi kwa ajili ya kusafirishia mazao bahari.

"Kama mnavyofahamu nchi yetu imebarikiwa kijiografia tunafanya hivyo kwasababu tunauwezo wa kutumia rasilimali zilizopo kwenye maji zikaleta maendeleo nchini," amebainisha Mhagama.

Amesema kupitia shirika hilo vijana watapata ajira pamoja na uchumi wa nchi kuongezeka kutokana na biashara ya samaki itakayoenda kufanyika.

Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tafico, Dennis Simba amesema wamejipanga kuhakikisha miradi yote inatekelezwa ili kufungua uchumi wa buluu.