Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Samia awaonya bodaboda kutumika katika ujambazi

Muktasari:

  • Rais Samia Suluhu Hassan amewaonya baadhi ya waendesha bodaboda kuacha kutumika katika ujambazi pamoja na kukwapua mizigo ya watu ili kulinda heshima yao.

Dodoma. Rais Samia Suluhu Hassan amewaonya baadhi ya waendesha bodaboda kuacha kutumika katika ujambazi pamoja na kukwapua mizigo ya watu ili kulinda heshima yao.

Rais Samia ameyasema hayo leo Jumapili Julai 24, 2022 wakati alipompigia simu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka kuzungumza na madereva bodaboda na bajaji.

Madereva hao walikutana katika kongamano la kuimarisha ushiriki katika sensa ya makazi na watu ya mwaka 2022 jijini Dodoma ambapo pamoja na sensa watapata nafasi ya kueleza changamoto zao mbalimbali kwa Serikali.

Amesema baadhi ya madereva boda boda wamekuwa wakikwapua mizigo ya watu pamoja na vipochi hasa vya wanawake.

“Nyinyi ni maofisa usafirishaji wa kitaifa lakini baadhi yenu wanawaharibia sifa yenu kwa kutumika kukwapua na kupoteza mizigo ya watu lakini kutumika kwa ujambazi. Niwaombe jilindeni msipoteze sifa yenu nyie ni watu muhimu sana katika Taifa letu,”amesema.

Rais Samia amesema wanapozungumzia usafiri kwa wanyonge huo ni usafiri wao ambao unawezesha kusafirisha watu kwa bei nafuu.

Amesema sekta hiyo ni muhimu ambapo kati yao wamo wasomi wa kuanzia cheti hadi shahada.

“Mama yenu nipo pamoja na mtakayozungumza, RC ataniletea changamoto zenu ili tuweze kushughulikia,”amesema.

Kwa upande wake, Mtaka amesema washiriki wa kongamano hilo limejumuisha madereva bodaboda 4,000 kutoka nchini.

Amesema wawakilishi hao ni wawili kutoka kila mkoa, wawakilishi 30 kutoka katika kila wilaya za Mkoa wa Dodoma na Halmashauri ya Wilaya ya Dodoma 2000.

Amesema mashirika mbalimbali yaliyoshiriki Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF, Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (Tarura) na mabenki mengine.