Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sakata la maduka ya fedha za kigeni laibuka tena bungeni

Mbunge wa Viti Maalumu, Cecilia Paresso akizungumza bungeni alipokuwa akichangia mjadala wa kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa mwaka wa fedha 2022/2023 jijini Dodoma leo.  Paresso amehoji Serikali nini hatima ya wafanyabiashara wa maduka ya fedha za kigeni waliochukuliwa fedha na vifaa vyao na kikosi kazi kipindi cha utawala wa Awamu ya Tano. Picha na Edwin Mjwahuzi

Muktasari:

Mbunge wa Viti Maalum, Cecilia Pareso ameitaka Serikali kueleza hatma ya fedha na vifaa walivyovichukua katika maduka ya kubadilishia fedha za kigeni.

Dodoma. Mbunge wa Viti Maalum, Cecilia Pareso ameitaka Serikali kueleza hatma ya fedha na vifaa walivyovichukua katika maduka ya kubadilishia fedha za kigeni.

 Pareso amehoji hayo leo Juni7, 2022 wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa mwaka 2022/2023.

Amesema mwaka 2018, Serikali ilichukua fedha na vifaa vya maduka ya kubadilisha fedha za kigeni ikiwamo komyuta, mashine za EFD na baadhi ya wafanyabiashara walichukuliwa hati.

Amesema hiyo ni mara ya nne kutaka kupata kauli Serikali kuhusiana na wafanyabiashara hao ambao wameporwa fedha zao tangu mwaka 2018.

Hata hivyo, amesema hakuna muafaka wowote uliofikiwa kuhusiana na jambo hilo na kuitaka Serikali kueleza ni lini Serikali itafikia muafaka kuhusiana na mashauri ya wafanyabiashara hawo.

“Mmeunda taksi force mkaenda tena kwa wafanyabiashara kuwaambia kuwa mnadaiwa sasa mmechukua kila kitu halafu mnaenda kuwadai tena.

Mnafanya kazi kwa taksiforce ya kutishia watu na si kuleta muafaka ili watu wafanye biashara kwa amani na utulivu,”amesema.

Ameomba kupatiwa majibu ya Serikali ya kina na kweli kuhusu jambo hilo kwa kuwa wafanyabiashara hao wanataka kufahamu hatma mlizozichukua.