Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sabaya ataka kesi yake iharakishwe

Muktasari:

  •  Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya ameieleza Mahakama ya Hakimu mkazi Moshi kuwa anateseka gerezani kwa kuwa ni mgonjwa na akaomba upande wa mashtaka uharakishe upelelezi wa kesi dhidi yake.

  

Moshi. Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya ameieleza Mahakama ya Hakimu mkazi Moshi kuwa anateseka gerezani kwa kuwa ni mgonjwa na akaomba upande wa mashtaka uharakishe upelelezi wa kesi dhidi yake.

Huku akibubujikwa na machozi, Sabaya alisema gerezani si sehemu ya ‘picknic’.

Sabaya na wenzake wanne wanakabiliwa na mashtaka mbalimbali ikiwemo uhujumu uchumi na kujipatia Sh30 milioni kutoka kwa mfanyabiashara wa Bomang’ombe, Alex Swai aliyedaiwa kukwepa kodi.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Sylvester Nyegu, John Aweyo, Nathan Msuya na Antero Assey.

Kesi hiyo namba 2 ya 2022 yenye inasikilizwa na Hakimu Mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo, Salome Mshasha. Upande wa Jam huri una mawakili wanne Tumain Kweka, Khalili Nuda, Verediana Mlenza na Suzy Kimaro.

Hata hivyo, wakati wakili Mlenza akiomba kuahirishwa kwa kesi hiyo kutokana na upelelezi wa shauri hilo kutokamilika, Sabaya alinyoosha mkono mahakamani hapo na alipopewa nafasi alitoa ombi lake.

Ombi la Sabaya

“Mheshimiwa hakimu, kwa kuwa kesi hii ililetwa hapa Juni mosi mwaka huu na ikaelezwa mbele ya mahakama hii kuwa upelelezi umekamilika na mwendesha mashtaka akaomba tarehe ya karibu kwa ajili ya usikilizwahi wa kesi hii, kinachokwamisha kesi hii ni nini, tunaonewa, tunaomba Ofisi ya DPP ijue kinachofanyika kwenye ofisi yake.”

“Wakati tunaletwa Gereza la Karanga tulichukuliwa mazingira ya usiku na ya kutisha, tunaumia sana tunateseka na mimi ni mgonjwa, tuna imani na ofisi ya DPP ndiyo maana tunamuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aingilie kati kwa sababu tunaonewa,” alieleza Sabaya.

Wakili wa utetezi, Hellen Mahuna aliutaka upande wa mashtaka kuwa makini kwa kuwa ulishasema upelelezi umekamilika nna jana ukasema haujakamilika.

Hakimu anayeisikiliza kesi hiyo, Mshasha alisema hoja ya upande wa utetezi ni za msingi kwa kuwa awali upande wa mashitaka waliieleza mahakama kuwa upelelezi umekamilika.

“Nimesikiliza hoja za pande zote mbili,na hoja za upande wa utetezi ni za msingi na zina mashiko kwa hiyo naahirisha kesi hii mpaka Julai 4 mwaka huu angalau upande wa mashtaka uje na hitimisho,” alisema.