Sababu wajawazito kujifungua kabla ya wakati

Katibu wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Mkoa wa Pwani, Omary Punzi akimkabidhi sehemu ya msaada wa mavazi ya kusitiri watoto (Pampasi) Mkurugenzi Msaidizi wa huduma za Uuguzi Hospitali ya Mloganzila, Christina Mwandalima leo wakati wamaadhinisho ya siku ya watoto njiti iliyofanyika kwenye Hospitali hiyo. Picha na Sanjito Msafiri
Muktasari:
- Vyanzo vya wajawazito kujifungua kabla ya wakati vyaanikwa, Taasisi ya Mwalimu Nyerere yawafariji.
Kibaha. Kati ya wajawazito milioni 2 wanaojifungua kwenye Hospitali ya Mloganzila laki 2 wanajifungua watoto kabla ya wakati (njiti) huku sababu mbalimbali zikitajwa kuchangia hali hiyo ambazo ni pamoja na magonjwa yasiyoambukizwa na hata ukosefu wa lishe bora.
Hayo yamebainishwa leo ijumaa Novemba 17, 2023 na Mkurugenzi Msaidizi huduma za tiba wa Hospitali ya Mloganzira, Dk Faraja Chiwanga alipokuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya watoto njiti iliyofanyika kwenye hospital hiyo.
Amezitaja sababu zinazosababisha baadhi ya wajawazito kujifungua watoto kabla ya wakati (njiti) kuwa ni pamoja na kukabiliwa na maggonjwa yasiyo ya kuambukizwa pamoja na ukosefu wa lishe bora, huku akitoa wito kwa jamii kuzingatia ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya ili kuepuka changamoto hizo.
“Hata watoto wanaolazwa hapa mloganzira nusu yao ni wale waliozaliwa kabla ya wakati lakini kulingana na maboresho ambayo yameendelea kufanyika hivi sasa wanhudumiwa vizuri na wanakua nakufikia umri mkubwa kama ilivyo kwa wengi,”amesema.
Akizungumza kwenye hafla hiyo kabla ya kutoa msaada wa mahitaji muhimu kwa watoto njito kwenye Hospital hiyo ambayo wamerishikiana na wadau mbalimbali ikiwemo wakala wa Huduma za Misitu Kanda ya Mashariki (TFS) katibu wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Wilayani Kibaha Omary Punzi ameshauri wanawake waliojifungua watoto njiti wasikatishwe tamaa na hali hiyo kwani wana haki kama ilivyo kwa wengine.
“Sisi Taasisi ya Mwalimu Nyerere Wilaya ya Kibaha tumeshirikiana na wadau wengine kutoa misaada inayolenga kuwagusa watoto ambayo ni pamoja na saruji ambayo tumetoa Shule ya Msingi kambarage nguo za michezo huko mlandizi na hapa tumetoa mavazi ya watoto wachanga (pampas) na mafuta,”amesema.
Amesema kuwa kutoa msaada huo ni kuendelea jitihada za taasisi hiyo ambayo ni katika mapambano dhidi ya maadui watatu ambayo ni ujinga, maradhi na umasikini na katika kuadhimisha siku hiyo ya watoto njiti ambayo huwa inafanyika kila mwaka ifikapo Novemba 17.
“Tumeamua kuadhimisha siku hii ya watoto njiti kwa kutembelea hospitali hii na kuzungumza na uongozi pamoja na wanawake ambao walipia hatua ya kujifungua watoto kabla ya wakati ili kuikumbusha jamii kuwa changamoto hii bado ipo na inahitaji kuendelea kuifanyia kazi,”amesema.
Baadhi ya wanawake waliopitia changamoto ya kujifungua watoto njiti ambao walikuwa sehemu ya washiriki wa hafla hiyo wameushukuru uongozi wa hospitali hiyo kwa huduma nzuri walizozipta kipindi wakiwa wanahudumiwa baada ya kujifungua.
“Nilijifungua mtoto wangu kabla ya wakati ilikuwa miezi saba na nilikuwa nasumbuliwa na changamoto nyingi za kiafya, lakini baada ya kujifungua nilihudumiwa kikamilifu na mpaka sasa mtoto wangu huyu hapa anaendelea na afya njema,”amesema Ester Kesy.
Jeny Mkombozi amesema kuwa wakati akijifungua motto wake hakuwa na uhakika kama angekua na hali aliyonayo sasa lakini hayo yote ni kutokana na jitihada za wafanyakazi wa hospitali hiyo.