Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rungwe wazalisha chai kilo 23 milioni kwa mwaka

Ofisa mradi  Mwandamizi wa Shirika la IDH, Michael Joseph alitoa maelekezo ya mradi wa mafunzo ya shamba darasa kwa wakulima wadogo wa chai  ulionufaisha wakulima 792  kutoka halmashauri za Rungwe na Busokelo  Mkoa wa Mbeya. Picha na Hawa Mathias

Muktasari:

  • Uzalishaji huo umetokana na ongezeko la bei kutoka Sh320 kwa kilo hadi Sh366, hali iliyoleta msukumo kwa wakulima kuzalisha kwa tija sambamba na kufufua mashamba yaliyokufa.

Rungwe. Wastani wa kilo 23 milioni za majani mabichi ya chai zimezalishwa na wakulima wadogo kupitia vikundi 30 kutoka vijiji 22 chini ya vyama vya msingi vya ushirika (Amcos) vya Matebe na Kapugi Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya.

Mwenyekiti wa Wakulima Wilaya ya Rungwe, Issa Mwanyumba amesema leo Jumanne Agosti 29, 2023 kwenye mahafali ya mwaka mmoja  ya   mafunzo ya shamba darasa kwa wakulima 792 kupitia mradi wa Agri- Connect Boresha chai  unaotekelezwa na Shirika la IDH kwa ufadhili wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya  EU.

Amesema kitendo cha Serikali kuongeza bei ya zao hilo kimeleta neema kwa wakulima kufufua mashamba ambao yalikuwa yametelekezwa.

Pia wamepongeza wa mradi wa IDH kuwashika mkono kwa kutoa elimu ya matumizi ya teknolojia za kisasa katika uzalishaji kwa kuondoa vikwazo kwa wakulima.

“Mradi huu wa mwaka mmoja umeleta matokea makubwa kwenye kilimo cha chai, kwani pamoja na Serikali kuongeza bei ya unununuzi kwa kilo kutoka Sh320 mpaka 366 uzalishaji wake kwa msimu uliopita   umekuwa kwa kasi tofauti na miaka ya nyuma.

Amesema awali katika miaka ya nyuma wakulima wengi walikata tamaa na kujikuta wakitekeleza mashamba kutokana na changamoto ikiwepo ukosefu wa pembejeo za kilimo kwa wakati, vifaa vya kisasa sambamba na mashine kwa ajili ya kuchuma chai mbichi mashambani.

“Mapema Januari 18 mwaka huu viongozi wa Amcos za wakulima tulishiriki mkutano wa wadau wa kilimo Mkoa wa Iringa, ambapo Serikali ilitangaza ongezeko la bei ya chai kwa kilo moja kutoka Sh 320 mpaka 366 jambo ambalo wakulima walilipokea kwa shangwe,” amesema.

Kwa upande wake, ofisa mradi mwandamizi wa IDH, Michael Joseph amesema mradi huo wa mwaka mmoja na uliowafikia wakulima 792 kwenye halmashauri ya Rungwe na Busokelo ulilenga kuwajengea uwezo wakulima wadogo wa chai kuzalisha kwa tija na kupata masoko ya uhakika.

Amesema lengo la mradi huo ni kuwafikia wakulima 10,000 watakaogawanywa katika awamu mbili lengo ni kuboresha sekta ya kilimo kupitia program ya mashamba darasa ambayo yataleta tija kubwa katika uwekezaji wa sekta ya kilimo Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya.

Amesema mikakati katika programu ya mradi wa shamba darasa utakuwa endelevu kwa kipindi cha miaka minne ambapo utalenga kwa wakulima wadogo kuwajengea uwezo wa kuzalisha mazao mbadala ikiwepo masuala la lishe bora.

“Hawa wakulima waliohitimu leo wamepata elimu ya miezi 12 kwa mfumo wa mashamba darasa kupitia vikundi vya wakulima kati ya 25 mpaka 30 sambamba na kuwapatia nyenzo za kujifunzia hususan uwezeshwaji kwa maofisa ugani,” amesema.

Naye Kaimu Mkurugenzi halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, Ally Said amesema Serikali itaendelea kuunga mkono juhudi za wadau wa kilimo katika suala zima la kuleta mageuzi katika sekta ya kilimo cha chai wilayani humo.

“Serikali itaendelea kushughulikia changamoto kwa kuboresha kilimo cha chai ikiwepo tatizo la ukosefu wa vifaa vya kisasa vya uchumaji wa majani mabichi ya chai kwa kushirikiana na Wizara ya kilimo,” amesema.