Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ripoti yaibua mapya taka zinazooza Dar

Wakusanya taka wa sekta isiyo rasmi (waliovaa fulana za njano) Kurasini, Temeke, wakionyesha taka zilizotengwa tayari kwa kukabidhiwa kwa mkusanyaji mkuu eneo hilo. 

Muktasari:

  • Wadau washauri kampeni za mazingira zizingatie athari za mabadiliko ya tabianchi

Dar es Salaam. Wakati ripoti mpya ikionyesha asilimia 63.4 ya taka zinazozalishwa jijini Dar es Salaam ni zinazooza, wadau wameshauri kampeni za kukabiliana nazo ikiwa moja ya njia za kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi.

Taka hizo ambazo kwa kiasi kikubwa zinatokana na mabaki ya chakula na matunda, zinapooza hutoa gesijoto kama methane na kaboni, hivyo kuchochea mabadiliko ya tabianchi na mafuriko pale zinapoziba mifereji wakati wa mvua.

Ripoti ya Dar es Salaam Urban Resilience Project (DURP) ya Machi 13, 2024 inaeleza, “taka hizo husababisha mabadiliko ya tabianchi, zisizodhibitiwa huachwa kando mwa barabara, mito au mifereji, zikiharibu mazingira.”

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, asilimia 57 ya taka jijini Dar es Salaam huishia mitaani kati ya tani 5,300 zinazozalishwa kila siku, huku tani 1,500 pekee zikifikishwa dampo. Kati ya taka hizo, zaidi ya asilimia 60 ni zinazooza.

Ripoti ya Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) inaonyesha tani bilioni 1.3 za chakula hupotea kila mwaka, na kuzalisha tani bilioni 3.3 za gesijoto, sawa na asilimia nane hadi 10 ya uzalishaji wa gesijoto duniani.

Wadau wanapendekeza mikakati madhubuti ya urejelezaji na utengenezaji wa mbolea kutokana na taka zinazooza ili kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi.


Udhibiti wa taka

Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004 kifungu cha 114 inazipa wajibu wa kutekeleza mamlaka ya serikali za mitaa kusimamia na kupunguza taka. Kwa kiwango kikubwa huzalishwa majumbani na sokoni.

Wakusanya taka wa sekta isiyo rasmi (waliovaa fulana za njano) Kurasini, Temeke, wakionyesha taka zilizotengwa tayari kwa kukabidhiwa kwa mkusanyaji mkuu eneo hilo. 

Kiongozi wa tafiti na mshauri wa masuala ya maendeleo, Mansoor Ali anasema wamefanya tafiti sita kwenye mradi wa DURP mwaka 2024 kwa ufadhili wa Serikali ya Uingereza.

Anasema miongoni mwa maeneo waliyoyabaini ni kuwajengea uwezo wasimamizi wa taka wa manispaa ili kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi.

“Wasimamizi wa taka waachane na mnyororo uliozoeleka wa usimamizi wa taka unaoanza na uzalishaji kisha mkusanyaji anayepeleka dampo, badala yake taka zitenganishwe kwenye chanzo na zifanyiwe kazi kulingana na aina yake. Hili linaongeza thamani ya taka na kupunguza athari za mazingira,” anasema.

Mansoor anasema maofisa hujengewa uwezo mara chache, pasipokuwa na mwendelezo, hivyo kuwapo tatizo katika utekelezaji.

“Tumewajengea uwezo maofisa zaidi ya 20, ambao tunatarajia wakaboreshe kampeni za mazingira zilizopo na watakazobuni zijumuishe masuala ya mabadiliko ya tabianchi ili kuendana na hali halisi ya dunia kwa sasa,” anasema.


Elimu inatolewa

Akizungumzia elimu waliyopewa, kiongozi na mwakilishi mkuu wa maofisa hao, Geophrey Zenda anasema: “Taka hasa za kuoza zinazalisha hewajoto ambazo ni hatari kwa mazingira. Katika elimu tunazotoa ni utenganishaji taka, udhibiti mzuri na kuchakata zile zinazowezekana.”

Wananchi wa Vingunguti na wadau wakifanya usafi wa katika daraja la Kwa Kombo. Usafi huu ulilenga kusafisha mifereji, madaraja ili kupunguza athari za mafuriko na mazingira.

Zenda, ambaye pia ni ofisa afya mazingira mkuu katika Wilaya ya Ilala, anasema walijifunza zaidi udhibiti wa taka unavyofanyika maeneo mengine duniani kabla ya kuja kuwaelekeza wenzao nchini.

Anasema Pune, nchini India wakusanya taka wa sekta isiyo rasmi walisajiliwa tangu 2008, wakisaidia kukusanya na kuzitenganisha kabla ya manispaa kuzikusanya. Pia, matumizi ya nishati itokanayo na taka (biogas) yanahamasishwa katika kaya na migahawa kama nishati mbadala.

Zenda amesema mafanikio yanategemea ushirikishwaji wa jamii, takwimu sahihi, miradi bunifu, ushirikiano wa sekta binafsi, uwezeshaji wa wafanyakazi wa sekta isiyo rasmi, sera bora, tathmini ya miradi na mabadiliko ya tabia.


Kampeni za halmashari

Kampeni za halmashari

Wananchi wa Kata ya Mji Mwema Kigamboni – walifanya kampeni ya “Usafi ni mimi na wewe” Machi 12,2024 walifanya usafi katika soko la Ungindoni na maeneo ya mtaa huo.

Zoezi hilo limeongozwa na Ofisa Afya na Mazingira wa Halmashauri ya Kigamboni, Sixbert Kyaruzi, aliyesisitiza umuhimu wa usafi hasa msimu wa mvua unapokaribia ili kuepuka magonjwa ya mlipuko.

Pia amewahimiza, “Tutenganishe taka kwa kuwa baadhi zinaweza kuuzwa au kutumika kama mboleana nyingine zinaweza kuuzwa zlivyo”.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Ungindoni, Shakukle Jafari, amepongeza juhudi za wananchi katika kuhakikisha soko linakuwa safi, akisisitiza kuwa eneo hilo huzalisha taka kwa wingi.

Mfanyabiashara wa nyanya, Devotha Zakayo, amekubaliana na zoezi hilo lakini aliomba mamlaka kuondoa taka kwa wakati ili kuepusha harufu mbaya.

Aidha, Ofisa Afya wa Kata ya Mji Mwema, Alnur Mshana, ametoa elimu kuhusu ugonjwa wa Mpox, akiwataka wananchi kujua dalili na jinsi ya kujikinga.

"Nadhani mnajua kama Kuna ugonjwa umeingia hapa nchini unaitwa mpox hivyo ni vyema wananchi kuchukua hatua juu huu, kujua dalili na namna ya kujikinga kwake," amesema Mshana.

Temeke na utoaji elimu, “Badili tabia, badili taka kuwa mali”

Wananchi wa Kurasini, Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam, walipewa elimu kuhusu fursa zilizopo kwenye taka kupitia kampeni ya mazingira iliyofanyika Machi 14 na 15, 2025 kwenye kata hiyo.

Elimu hiyo ilitolewa na wadau wa mazingira wakiongozwa na Ofisa Afya wa Kata ya Kurasini, Imani Mohamedi Rajabu, kwa kushirikiana na kampuni za wadau wengine wa mazingira.

"Hapa leo tumetoa elimu jinsi ya kutumia takataka kwa ajili ya kuboresha maisha na mazingira yetu ya kila siku," amesema Rajabu

Rajabu alisisitiza kuwa taka si uchafu bali ni mali inayoweza kuleta kipato, akisema wamefundisha wananchi jinsi ya kuzitumia taka kuboresha maisha na mazingira yao.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mivinjeni, Mwamtum Gumbo, “Elimu hii itakwenda kupunguza taka mtaani kwani hapo awali wananchi waliona kama haiwezekani taka kuwa mali, kizuri zaidi hapa mtaani kuna mtu ameanzisha kiwanda kidogo cha kununua taka hali hio imekuja kuleta hamasa zaidi”.

Mmiliki wa kiwanda hicho, Dotto Maliatabu, alisema licha ya mchango wake katika kuchakata taka, anakumbana na changamoto kutoka kwa baadhi ya viongozi wa serikali wanaodai anachafua mazingira.

Hata hivyo, amekuwa akielimisha viongozi hao juu ya umuhimu wa shughuli yake katika usafi wa mazingira.

Mmoja wa muokota taka Kurasini Saidi Fadhiri anasema, “…pamoja na kujiajiri kwa kuokota taka lakini kuna baadhi ya watu wanatuona kama wezi wa mtaani lakini sio kweli, sisi tunachangia kuweka mazingira sehemu salama, na hii ni ajira tunaendesha maisha na familia kwa kazi hii”.

“Safisha pendezesha jiji” ya Ilala

Wakazi wa Mtaa wa Kwa Kombo Vingunguti jijini Dar es Salaam wamefanya usafi katika madaraja ya mtaa huo pamoja na soko la kwa Simba ikiwa ni kampeni maluum ya kusafisha mitaro kwa ajili kujiandaa na mvua zinazotarajia kunyesha hivi karibuni.

Usafi huo umefanyika chini ya uangalizi wa Ofisa afya wa kata ya vingunguti, Amisa Mtendawema Marchi 15, 2025 huku vikundi mbalimbali vya kijamii vikijitokeza kushiriki kufanya  usafi katika mtaa huo.

Amisa alisema wamefanya hayo kujiandaa na mvua zinakuja na kusababisha mafuriko. “Tunafahamu uchafu unaziba mitaro na njia ya maji, hili linachochea athari za mafuriko na kutishia uwepo wa magonjwa ya mlipuko”.

Kwenye usafi huo kulikuwa na zaidi ya wananchi 100 waliojitokeza. “Kabala ya leo kuja hapa kwa wingi tulianda kampeni maluum kwa wadau wa mazingira na wananchi kuhamasisha ushiriki wao. Na tunashukuru wamejitokeza”.

Kwa upande wake mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kwa Kombo Athumani Musa, amesema usafi uliofanyika kwenye soko la Kwa Simba ni muhimu kwani soko hilo halina mkandarasi maalumu kwa kukusanya taka.

Kikundi cha Ilala Jogging, kikiongozwa na Hassani Samakimkubwa, kimeshiriki usafi Vingunguti ili kuzuia magonjwa ya mlipuko. Samakimkubwa amesema kampeni yao ya usafi wa kila wiki imepunguza milipuko ya magonjwa kama kipindupindu, hasa katika msimu wa mvua.

Kinondoni na Ubungo

Halmashauri ya Kinondoni walitekeleza kampeni ya “Mguu kwa mguu kitaa” na kufanya usafi katika mtaa Kwa Kopa Mwananyamala Mach 18, 20245 ambapo walitembelea nyumba kwa nyumba kwenye kwenye mtaa huo udhibiti wa taka kuanzia majumbani.

Ofisia Mazingira na Afya wa Kindoni, Alban Mugyabuso alitaja malengo ya mradi huo ni kuongeza uelewa, kusafisha mazingira, kukabili magonjwa ya milipuko na kuongeza uchumi wa wananchi kwa kuongeza thamani ya taka.

Halamashauri ya Ubungo iliyowakilishwa na Ofisa Usimamizi wa Mazingira (EMO) Anna Kitutu ilitaja kuendeleza kampeni yake ya, “KAUSAPEU” yenye maana ya Kataa Uchafu, Safisha Pendezesha Ubungo.

“Tunapanga kutumia kituo cha Mabasi cha Magufuli kwa kutumia kipaza sauti kuhamaisha uhifadhi wa mazingira na kufanya usafi pamoja na wananchi” alisema.