RC Iringa amewataka wananchi kuacha ujangili


Muktasari:

  • Halima Dendego amewaagiza wananchi wa Kijiji cha Makifu Tarafa ya Isimani kuachana na vitendo vya ujangili na uharibifu wa hifadhi, hii imetokana na athari zilizowakumba kijiji hicho kwa sasa.

Iringa. Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Halima Dendego amewataka wakazi wa Makifu kuacha tabia ya kutaka kujitwalia mali bila kibali chochote na kuagiza mhalifu akibainika akamatwe.

Dendego amesema watu waliofanya hivyo wamesababisha changamoto kwenye maji, misitu na mbuga na mara nyingi elimu imekua ikitolewa japokuwa bado kuna wimbi la wahalifu.

Aliongeza kwa kusema Serikali ya Mkoa itaendelea kutoa elimu na wahalifu sugu watakaokamatwa  hatua zaidi zitachukuliwa  na wanaandaa namna ya kufanya utafiti kwa pamoja na Hifadhi ya Taifa Tanzania (Tanapa) pia raia wema ili kunusuru uoto wa asili.

"Kwa wanaoendelea kuvunja sheria tumejipanga kuwachukulia hatua na kurudisha hali ya mazingira safi tutapanda miti," amesema Dendego.


Diwani Viti Maalumu Tarafa ya Idodi, Shany Richard amesema hifadhi ni faida kwa wanakijiji kwa kupata mvua na mazingira kuwa safi hata athari za leo zisingepatikana kama wananchi wanalinda mali hizo.

Naye Mkuu wa Hifadhi ya Ruaha, Godwel Ole Meing'ataki amesema pia kuna majangili wa uvuvi wa samaki wanaoharibu Hifadhi ya Ruaha, Mto Ihefu.

"Mimi nalibeba hili kwani linasikitisha sana na viongozi msilikumbatie jambo hilo," amelisema Meing'ataki.

kwa upande wa wananchi wa kijiji hicho  wamesema baadhi ya viongozi ndio wanaoongoza kufanya uharibifu katika hifadhi.

''Leo imekuwa kama injili ya watu tuache dhambi lakini wananchi tunaomba sisi wenyewe tubadilike,"alisema Agnes Nzale.