Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Samia atoa maagizo kwa viongozi wa dini

Rais wa Jamhuri Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia viongozi mbalimbali pamoja na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Baraza la Maulid la kusherehekea mazazi ya Mtume Muhammad (S.AW) ambalo Kitaifa limefanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Oktoba, 2022.

Muktasari:

  • Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza suala la maadili kwa watoto akilitaka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) na viongozi wa dini wengine kutoacha kulisemea.


Dar es Salaam.  Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza suala la maadili kwa watoto akilitaka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) na viongozi wa dini wengine kutoacha kulisemea.

 “Maadili haya ni mtetereko uliotokea ndani ya Taifa letu, kama wazazi, walezi na viongozi tulitetereka mahali. Turudi tukatizame wapi tulitetereka, tufundishan ili watoto wetu washike maadili.

“Waumini wa dini zote na Watanzania kuendelea kulichangia kwa kadiri mnavyoweza na Serikali ipo pamoja nanyi,” amesema Rais Samia wakati akishiriki sherehe za Baraza la Maulid zilizofanyika Jijini Dar es Salaam leo Jumapili.
 

Sherehe hizo zimefanyika  leo Jumapili  Oktoba 9,2022 na zilihudhuriwa pia viongozi wengine akiwemo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson, Sheikh Mkuu Abubakar Zubeir pamoja,  viongozi wa ulinzi na usalama, wabunge na mawaziri.


Akizungumzia maovu ya mauaji, ikiwemo ya watoto wachanga hasa wa kike wanaonekana hawana thamani katika jamii kama wa kiume, kudhulumiana, kudhauliana, kuhujumiana, Rais Samia amesema bado yapo dunia na katika Taifa hili, akiwatak viongozi wa dini wakayafanyie kazi.


Rais Samia amesema Serikali itayafanyia kazi kwa upande wake kadiri inavyoweza, lakini viongozi wa dini wakayasemea ili kupunguza changamoto hiyo, itakayosaidia kuendana na mienendo iliyowekwa katika dini.


“Ikiwa leo tunasherekea ni vema tukamuenzi Mtume kwa mafundisho aliyokuja nayo kwa Waislamu na wananchi wote pamoja na kutafakari hali yetu katika jamii na tunavyoishi. Tumekuwa tukishuhudia vitendo vingi viovu ambavyo hawezi kufumbiwa macho na lazima tupambane kuvitokomeza.


“Natoa wito kwa viongozi wa dini kwenda kulifanyia kazi suala hili kwa maslahi mapana ya Taifa letu.Wakati wa kuadhimisha Maulid ni wakati wenye mafunzo makubwa kwa Waislamu na wasio waislamu, kwa sababu matendo maovu na yasiyo maobu hayategemei dini yanayaweza kufanywa na yeyote,”amesema Rais Samia.


Amesema matendo maovu yanayofanyika athari yake inakuwa kwa kila mtu bila kujali dini sambamba na vitendo vizuri. Amewataka viongozi hao kuhimiza waumini wao kwa kusimama na matendo mema sambamba na kuendeleza mafunzo ya dini zao.


Kuhusu changamoto ya muda mdogo wa watoto wa kuhudhuria madrasa, Raisa Samia amesema Serikali ina mpango wa kubadilisha mtaala wa Tanzania, kwa sasa inakusanya maoni ya Watanzania kuhusu mchakato huo, akisema anaamini Bakwata watalifikisha suala hilo.


“Wakati sisi tulipapata nafasi ya kuhudhuria madarasa shuleni ilikuwa mwisho saa saba, unarudi nyumbani unajimwahia maji unaambiwa nenda madrasa. Lakini wakati umebadilika, wakati ule sio huu, sasa hivi mambo ni mengi na idadi ya watoto ni kubwa, madrasa yanajaa kuna wanafunzi wengine wanaingia awamu mbili.


“Lakini tujipange katika teknolojia ili kuwafundisha watoto kwa muda watakaokuwa nyumbani. Wale watakaowahi madrasa waende, wale watakaochelewa basi tutumie sayansi na tuwe na vipindi maalumu vya dini,” amesema Rais Samia.