Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Samia ateua, kuhamisha Ma-DC, DED, DAS na bosi Tanapa

Muktasari:

 Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameendelea kupanga safu za wasaidizi wake kwa kuteua na kuhamisha vituo vya kazi baadhi yao.

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameendelea kupanga safu za wasaidizi wake kwa kuteua na kuhamisha vituo vya kazi baadhi yao.

Mara hii, amewagusa wakuu wa wilaya (DC), Wakurugenzi wa Halmashuri (DED), Makatibu Tawala wa Wilaya (DAS) na kuteua kaimu kamishna wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa).

Kama kawaida ni mwendo wa usiku kwa usiku kwa maana ya mabadiliko hayo yametangazwa usiku wa leo Jamanne, Oktoba 3, 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus.

Mara hii uteuzi huo umefanyika wakati Rais Samia akiwa Doha, nchini Qatar alikoshiriki Maonyesho ya Kimataifa ya Mboga na Matunda 2023 kwa lengo la kutafuta fursa mbalimbali za masoko ya mazao ya kilimo.

Rais Samia aliwahi nukuliwa hivi karibuni akiwaeleza wasaidizi wake anaendelea kupanga-pangua hivyo wakachape kazi lasivyo watamwona Zuhura akitangaza mabadiliko hayo usiku na wakiamka watajisoma mtandaoni.


Undani wa mabadiliko hayo ni kama ifuatavyo:-

i. Amemhamisha kituo cha kazi Sixtus Raphael Mapunda kutoka Wilaya ya Sumbawanga kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke.

Mapunda anachukua nafasi ya Mobhare Matinyi ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari - Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali.

ii. Amemhamisha kituo cha kazi Mkuu wa Wilaya ya Urambo, Kenan Laban Kihongosi kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Momba mkoani Songwe.

Kihongosi anachukua nafasi ya Fakii Lulandala ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu UVCCM.

iii. Amemteua Elibariki Bajuta, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro kuwa Mkuu wa Wilaya ya Urambo mkoani Tabora badala ya Kenan Kihongosi ambaye amehamishiwa Momba.

iv. Amemteua William Mwakilema, Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa) kuwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga.

Mwakilema anachukua nafasi ya Jokate Mwegelo ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT).

v. Amemteua Nyakia Chirukile kuwa Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga akichukua nafasi ya Sixtus Mapunda aliyehamishiwa Wilaya ya Temeke.

Kabla ya uteuzi huo Nyakia alikuwa Katibu Tawala wa Ngorongoro.

vi. Ametengua uteuzi wa Halfan Magani, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Korogwe na badala yake kumteua Goodluck Mwangomango.

Kabla ya uteuzi huo Mwangomango alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Singida.

vii. Amemteua Said Majaliwa kuwa Mkurugenzi wa Tanga Mjini. Kabla ya uteuzi huo Majaliwa alikuwa Mkurugenzi Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga.

viii. Amemeteua Faraja Msigwa kuwa Mkurugenzi wa Kilindi Mkoani Tanga. Kabla ya uteuzi huo Msigwa alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Karatu mkoani Arusha.

ix. Amemteua Naima Chondo kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Singida Mjini. Naima anachukua nafasi ya Goodluck Mwangomango ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Wilaya ya Korogwe.

x. Amemteua Shamim Sadiq kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Ruangwa.

xi. Amemteua Hamza Hamza kuwa Katibu Tawala Wilaya ya Ngorongoro ambapo anachukua nafasi ya Nyakia Chirukile ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga.

Kabla ya uteuzi huo Hamza alikuwa Ofisa Tarafa wa Ngudu, Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza.

xii. Amemteua Lameck Ng'ang'a kuwa Katibu Tawala Wilaya ya Karatu mkoani Arusha.

Ng'ang'a ambaye alikuwa Katibu Tarafa Karatu anachukua nafasi ya Msigwa aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilindi.

xiii. Amemteua Musa Kuji kuwa Kaimu Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi ya Taifa Tanzania (Tanapa).  Kuji alikuwa Naibu Kamishna wa Huduma za Shirika (TANAPA).