Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Samia aendeleza ndoto ya Magufuli kwa uzinduzi wa Daraja la JPM

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya ujio wa Rais Samia Suluhu Hassan mkoani humo.

Muktasari:

  • Daraja la Kigongo-Busisi linaunganisha mikoa ya Mwanza na Geita kupitia Ziwa Victoria na ni miongoni mwa madaraja marefu zaidi Afrika Mashariki na Kati.

Mwanza. Uzinduzi wa Daraja la JPM (maarufu kama Daraja la Kigongo–Busisi) utakaofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan ni tukio la kihistoria linalobeba uzito mkubwa katika maendeleo ya kitaifa, hasa kwenye sekta ya miundombinu.

Daraja la JPM ambalo ni maarufu kama Kigongo-Busisi linaunganisha eneo la Kigongo Wilaya ya Misungwi na Busisi Wilaya ya Sengerema.

Kukamilika kwa daraja hilo lililojengwa kwa gharama ya zaidi ya Sh700 bilioni kutarahisisha ussfirishaji siyo tu kwa mikoa ya Geita, Kagera, Mwanza na Kigoma na nchi jirani za Uganda, Rwanda, Burundi na DRC kwa kumaliza kero ya muda mrefu uliokuwa ukitumika kuvuka kwa kutumia vivuko vya MV Mwanza na Mv Misungwi.

Kwa kuzindua daraja hili, Rais Samia anadhihirisha dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuendeleza miradi ya kimkakati iliyoanzishwa na mtangulizi wake, Hayati Dk John Magufuli.

Hii ni ishara ya uendelevu wa sera na mikakati ya maendeleo, pamoja na kuthibitisha kwamba Serikali ipo makini katika kuwekeza kwenye miundombinu inayogusa maisha ya watu moja kwa moja.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya ujio wa Rais Samia Suluhu Hassan mkoani humo.

Daraja hili litaongeza kasi ya biashara, kuinua uchumi wa wakazi wa Kanda ya Ziwa, na kuvutia wawekezaji kwa kurahisisha usafirishaji wa bidhaa na huduma.

Hivyo basi, uzinduzi huu si tu ishara ya mafanikio ya kisera, bali pia ni hatua ya dhati kuelekea uchumi jumuishi na endelevu.


Rais Samia ziarani Mwanza, Simiyu

Kwa upande wa Serikali ya Mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda, amesema  Rais Samia anatarajiwa kutua katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza kesho (Juni 15, 2025)   kabla ya kuelekea mkoani Simiyu kwa ziara ya siku tatu, kisha atarejea Mwanza Juni 19, 2025 kwa ajili ya kuzindua Daraja la JPM maarufu kama Kigongo-Busisi.

Baada ya uzinduzi wa daraja hilo, Rais Samia atazungumza na wananchi katika eneo la Chuo cha Ufundi Kalwande, kilichopo Bukumbi, Wilaya ya Misungwi.

Aidha, Juni 20, mwaka huu atazindua mradi mkubwa wa maji Butimba wenye thamani ya Sh71 bilioni, unaotarajiwa kuhudumia wakazi 450,000 wa Jiji la Mwanza na viunga vyake kwa kuzalisha lita milioni 48 za maji kwa siku.

“Juni 20, Rais Samia Suluhu Hassan atashiriki kwenye uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa chanzo kipya cha maji Butimba na kituo cha kusafisha na kutibu maji na kisha kushiriki kwenye Siku ya Walinzi wa Jadi (Sungusungu) katika Viwanja vya CCM Kirumba, pia tunawakaribisha wananchi kushiriki mkutano huo,” amesema.

Juni 21, 2025, Rais atazindua Tamasha la Bulabo la utamaduni litakalofanyika Uwanja wa Red Cross, Bujora wilayani Magu ambalo tayari lina wiki moja tangu limeanza.

Pia, Mtanda amewaonya watu wenye nia ovu dhidi ya kuvuruga ziara ya Rais Samia akisema, Serikali haitavumilia vitendo vyovyote vya uchochezi au uvunjifu wa amani.

Amesema wananchi wanaruhusiwa kubeba mabango yenye ujumbe wa pongezi au kuwasilisha kero zao kwa njia ya heshima, lakini amesisitiza kuwa vitendo vyenye kwenda kinyume na maadili havitavumiliwa.

“Lakini vitendo ambavyo vipo kinyume na maadili haviruhusiwi na nitumie fursa hii kuwataka wana Mwanza kuonesha uungwana, kuonesha mapokezi makubwa, kwa kazi kubwa ambayo Rais ameifanya,”amesema.


 Ziara ya Rais Samia Simiyu

Katika ziara yake hiyo ya kwanza mkoani Simiyu tangu aingie madarakani mwaka 2021, Rais Samia atatembelea wilaya za Maswa, Meatu, Bariadi, Itilima, Busega na Bariadi Mjini kuanzia Juni 16, 2025.

 “Migogoro kati ya viongozi wa CCM na wale wa Serikali imekuwa kikwazo kwa shughuli za maendeleo. Tunataka kuona mshikamano,” amesema Leonard Paul, mkazi wa Bariadi Mjini.

Joyce Yohana, mkulima kutoka Kijiji cha Nyabubinza wilayani Maswa, amesema: “Rais Samia anakuja wakati tunahitaji majibu. Tunahitaji kusikia kuhusu bei ya pamba, matumizi ya mizani na hali ya barabara zetu. Huu si wakati wa hotuba tu, bali utekelezaji.”

Wananchi wa Maswa pia wanatarajia kupata majibu kuhusu kiwanda cha chaki cha halmashauri hiyo, ambacho licha ya kugharimu Sh12 bilioni za Serikali, bado hakijaanza uzalishaji kutokana na ukosefu wa mtaji.

Katika Wilaya ya Meatu, wakulima wa mbaazi na alizeti wamelalamikia ukosefu wa soko la uhakika, pamoja na ucheleweshwaji wa ujenzi wa barabara ya kutoka Mwanhuzi hadi Bukundi ambayo imekuwa kilio cha muda mrefu.

“Tulihamasishwa kulima mbaazi na alizeti, lakini hakuna soko la uhakika. Na kuhusu barabara ya Mwanhuzi–Bukundi, tunaambiwa ipo kwenye ilani ya chama lakini hadi leo hakuna hata kipande cha lami,” amesema Maiko Mayunga, mkazi wa Kijiji cha Nkoma.