Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Mwinyi kuzindua taasisi ya kuratibu, usimamizi kazi serikalini

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi

Muktasari:

  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi, kesho Ijumaa Desemba 2, 2022 anatarajiwa kuzindua Taasisi ya Ufuatiliaji na Usimamizi utendaji kazi Serikalini (Presidential Delivery Bureau) hafla itakayofanyika Ikulu, Zanzibar.

Unguja. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi, kesho Ijumaa Desemba 2, 2022 anatarajiwa kuzindua Taasisi ya Ufuatiliaji na Usimamizi utendaji kazi Serikalini (Presidential Delivery Bureau) hafla itakayofanyika Ikulu, Zanzibar.

  

Akizungumza Ikulu kuhusu uzinduzi wa taasisi hiyo leo Alhamisi Desemba Mosi, 2022 Ikulu Zanzibar, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Charles Hillary amesema lengo la taasisi hiyo mpya ni kuratibu utendaji unavyotakiwa uende kwa haraka na kwa ufanisi zaidi.


“Hii taasisi ni mpya na imeanzishwa na Rais mwenyewe, kwahiyo bado hata watendaji wahawajaielewa lakini wanapewa mafunzo,” amesema


Amesema jumla ya watu 250 watahudhuria hafala hiyo ikiwa ni pamoja na mawaziri, manaibu wao na makatibu wakuu na watendaji wakuu wa taasisi za SMZ na takribani mabalozi 20 wanaoziwakilisha nchi zao nchini Tanzania.


Akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo na uelewa kuhusu taasisi hiyo Mawaziri na watendaji mbalimbali, Waziri wa Nchi (OR) Ikulu, Jamal Kassim Ali katika ukumbi wa Sheikh idrissa Abdul-wakil Kikwajuni, amesema PDB itakuwa jukumu la kusimamia masuala yote kuhusiana na utekelezaji wa vipaumbele vya mipango na mikakati  ya Serikali.


Amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uelewa viongozi na watendaji hao ili kufahamu madhumuni, majukumu na kwa namna gani chombo hicho kitafanya kazi zake.


Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo ya PDB, Dk Josephine Kimaro, amesema utekelezaji wa vipaumbele vya miradi ya Serikali utahusika katika maeneo makuu manne; sekta ya uchumi wa buluu, utalii, miundombinu na maendeleo ya kijamii.


Amesema utekelezaji wa vipaumbele vya miradi ya Serikali kupitia wizara kwa kiasi kikubwa vina mnasaba na mikakati mbalimbali ya Serikali.


Mtendaji huyo ameeleza umuhimu wa kuwepo ushirikiano wa karibu katika utekelezaji wa vipaumbele hivyo kati ya Wizara za Serikali, kwa kuzingatia kuwa utekelezaji wa baadhi ya miradi unahusisha zaidi ya Wizara moja.


Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi, Mhandisi Zena Said amesema kuanzishwa kwa taasisi hiyo kutakuwa chachu kwa watendaji wa Serikali kutekeleza majukumu yao kwa wakati na kwa weledi.


Alipongeza Taasisi ya Tony Blair kwa kusaidia uanzishaji wake, sambamba na kufanikisha utekelezaji wa vipaumbe  vya miradi ya Serikali kupitia maeneo yalioainishwa.