Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Samia ateua wenyeviti wa bodi


Muktasari:

  • Rais Samia aendelea kupanga safu yake akiteua wenyeviti wa bodi na mabaraza, amteua kwa mara nyingine Dk Kimirei kuongoza Tafiri.

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa  viongozi mbalimbali wa wenyeviti wa bodi na kumuongezea muda Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (Tafiri).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Moses Kusiluka, Dk Ismael Aaron Kimirei ameteuliwa kushika wadhifa  katika kipindi cha pili.

Naye Balozi Ernest Mangu ambaye ni Mkuu wa Jeshi la Polisi mstaafu ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA),  kwa kipindi cha pili.

Kwa upande wake Mkurugenzi mstaafu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dk Marina Njelekela ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI), akichukua nafasi ya  Profesa Charles Mkony ambaye amemaliza muda wake.

Uteuzi mwingine ni wa Juma Fimbo ambaye ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA).

Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Profesa James Mdoe ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) akichukua nafasi ya Dk Andrew Kitua ambaye amemaliza muda wake.