Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Raia wa Lithuania ahukumiwa maisha kwa dawa za kulevya

Raia wa Lithuania, Christina Biskavskaja (kushoto) akitoka Mahakama Kuu kanda ya Moshi, jana, baada ya kuhukumiwa kifungo cha maisha jela kutokana na kupatikana na hatia ya kusafirisha dawa za kulevya. Picha na Daniel Mjema

Muktasari:

  • Christina ambaye ni mwanamuziki katika Jiji la Kaunas, alikamatwa Agosti 28, 2012 saa tisa alasiri katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) akisafirisha gramu 3,775.26 za heroine zenye thamani ya Sh169 milioni.

Mahakama Kuu imemhukumu kifungo cha maisha jela raia wa Lithuania, Christina Biskavskaja baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha dawa za kulevya kwenda Ubelgiji.

Christina ambaye ni mwanamuziki katika Jiji la Kaunas, alikamatwa Agosti 28, 2012 saa tisa alasiri katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) akisafirisha gramu 3,775.26 za heroine zenye thamani ya Sh169 milioni.

Hukumu hiyo ilitolelwa jana na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, Aishiel Sumari aliyesema ushahidi wa mashahidi saba wa upande wa mashtaka ni mzito na umethibitisha shtaka dhidi ya mshtakiwa huyo.

Kesi hiyo iliendeshwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Tamari Mndeme aliyesaidiana na mawakili wa Serikali, Ignas Mwinuka na Sabitina Mcharo wakati mshtakiwa alitetewa na Patrick Paul.

Akisoma hukumu hiyo, Jaji Sumari alisema ushahidi wa upande wa mashtaka ulikuwa mzito na haukuacha shaka kuwa begi lililokuwa na dawa hizo lilikuwa la mshtakiwa.

Jaji Sumari aliukataa utetezi wa mshtakiwa kuwa alibambikiwa kesi hiyo na polisi wa Tanzania na kuhoji hilo linawezekanaje wakati mashahidi wa upande wa mashtaka walikuwa hawafahamiani na mshtakiwa.