Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Radi yaua mifugo Babati

Wakazi wa Kijiji cha Endamanang kata ya Nar wilayani Babati mkoani Manyara wakiangalia ng'ombe 16 na mbuzi watano waliokufa kwa kupigwa na radi.

Muktasari:

Ng'ombe 16 na mbuzi watano wa familia mbili tofauti kijiji cha Endamanang kata ya Nar wilayani Babati Mkoa wa Manyara imekufa baada ya kupigwa na radi iliyoambatana na mvua na upepo mkali.

Babati. Ng'ombe 16 na mbuzi watano wa familia mbili tofauti kijiji cha Endamanang kata ya Nar wilayani Babati Mkoa wa Manyara imekufa baada ya kupigwa na radi iliyoambatana na mvua na upepo mkali.

Hata hivyo, kwenye tukio hilo hakukuwa na madhara kwa binadamu zaidi ya kuzua hofu na taharuki kwa wakazi wa kijiji hicho.

Shuhuda wa tukio hilo, Richard Bayo akizungumza leo Jumatatu Machi 8, 2021 amesema tukio hilo limetokea Machi 7, 2021 na kubainisha kuwa tukio hilo limetokea wakati ng'ombe na mbuzi hao wakiwa wanachungwa kwenye eneo la malisho ya mifugo.

Amesema baadhi ya watoto wa eneo hilo walipatwa na hofu kutokana na mngurumo za radi na mvua iliyonyesha huku ikiambatana na upepo mkali.

"Tunamshukuru Mungu hakukuwa na madhara kwa binadamu zaidi ya ng'ombe na mbuzi hao kufa papo hapo wakati wa tukio hilo la kusikitisha," amesema Bayo.