Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Profesa Sarungi anavyozungumza mitandaoni

Profesa Phelemon Sarungi enzi za uhai wake. Picha na Mtandao

Muktasari:

  • Kupitia mitandao ya kijamii watu tofauti wamekumbushia matukio mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii aliyoshiriki kiongozi huyo  akitumia taaluma yake ya udaktari, akiweka kando nyadhifa zake alizokuwa nazo wakati huo.

Dar es Salaam. Unaweza kusema ’Historia haitomsahau’ huyo ni Profesa Philemon Sarungi (89) daktari bingwa wa mifupa nchini ambaye kupitia mitandao ya kijamii anatajwa ni kiongozi wa mfano.

Profesa Sarungi (89) aliyewahi kuwa  waziri wa wizara mbalimbali na mbunge wa Rorya, mkoani Mara aliyefariki dunia jijini Dar es Salaam  Jumatano Machi 5, 2025 nyumbani kwake Oysterbay wilayani Kinondoni jijini hapa.  Watu wanaomfahamu kupitia mitandao ya kijamii wameeleza  yaliyofanywa na kiongozi huyo.

“Kupitia mtandao wa X Nape Nnauye Mbunge wa Mtama ameandika “mwaka 2014 nilivunjika mkono, nilifanyiwa operesheni kubwa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) Baba Profesa Sarungi alinitembelea wodini karibu kila siku asubuhi kwa siku saba kuhakikisha hali yangu inatengemaa.

“Nakumbuka pia mapenzi yako kwa Simba, mzalendo mwema na hodari pumzika salama baba,” ameandika Nape kupitia mtandao wake wa X.

Kwa upande wake mfanyabiashara Mohammed Dewji kupitia mtandao wake wa X ameandika,

“Tanzania imepoteza kiongozi wa kipekee, nami nimempoteza rafiki mpendwa. Profesa Philemon Sarungi hakuwa tu daktari bingwa wa upasuaji na mzalendo wa dhati, bali pia mmoja wa wanachama waaminifu na wenye mapenzi makubwa kwa familia ya Simba SC,

 “Upendo wake na kujitoa kwenye klabu ya Simba vilidhihirika nilipopata heshima ya kumkabidhi Tuzo ya Maisha ya Simba. Tuzo aliyostahili kwa mchango wake mkubwa na wa kudumu kwa klabu yetu,

“Zaidi ya soka, Profesa Sarungi alikuwa nguzo muhimu katika sekta ya afya na utumishi wa umma nchini. Akiwa daktari bingwa wa upasuaji na mkufunzi mwenye weledi mkubwa, alileta mageuzi chanya katika huduma za afya Tanzania.

“Alitumika pia katika wizara mbalimbali, zikiwemo afya, elimu, uchukuzi na ulinzi, akitoa mchango wake wa thamani kwa Taifa.

“Pengo aliloacha ni kubwa, lakini urithi wake wa hekima na matendo mema utaendelea kuishi milele. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi,” amesema.

Ayubu Madenge aliandika “Mwaka 1992 mtoto mmoja wa miaka 10 alishambuliwa na mamba eneo la tumboni huko Rufiji Mkoa wa Pwani, akiwa anapelekwa hospitali alikutana na Profesa Sarungi wakati huo akiwa mkuu wa mkoa, Sarungi alisitisha ziara yake akaanza kumtibu mtoto huyo na akaokoa maisha yake,” ameandika Madenge.

Sio kwa tukio hilo tu, Godwin kupitia mtandao wake wa X alitaja tukio lingine Profesa Sarungi alihusika pia na matibabu ya waathirika wa ajali ya treni iliyotokea mkoani Dodoma.

Taarifa hiyo inaelezwa pia na Joe Boy aliyesema tukio hilo Profesa Sarungi alikuwa akielekea Dodoma na aliposikia ajali hiyo aligeuza msafara.

Tukio hilo pia linamkumbusha Mbunguni Timothy tukio la ajali ya iliyotokea mkoani Kagera wilayani Bukoba,

 “Miaka ya 1990 kulikuwa na ajali kule Bukoba jengo la shule liliwaangukia wanafunzi, Profesa Sarungi akiwa Waziri wa Elimu na daktari mbobevu wa mifupa aliwahi haraka eneo la tukio na kuwaongoza madaktari haraka kuwatibu watoto wale,” ameandika kupitia mtandao wake wa X.

Hilo pia linadhibitishwa na Japhet Mmbaga kupitia mtandao wake wa X akisema tofauti na wengine Profesa Sarungi aliingia chumba cha upasuaji moja kwa moja kufanya kwa vitendo  ‘sio unafika na kupigwa picha na  kusepa,’

Baba babu aliandika: Profesa Sarungi atakumbukwa kwa mazuri yake, huku Samson Ernest akieleza kuwa Profesa huyo alitumia taaluma yake kisawasawa.