Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Polisi yathibitisha Mwabukusi, Mdude wanashikiliwa kwa mahojiano

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, SACP David Misime

Muktasari:

  • Jeshi la Polisi linawashikilia Wakili Boniface Mwabukusi na Mpaluka Nyangali maarufu Mdude kwa mahojiano kutokana na maneno ya uchochezi wanayodaiwa kuyatoa.

Dar es Salaam. Jeshi la Polisi limethibitisha kuwakamata, linawashikilia Wakili Boniface Mwabukusi na Mpaluka Nyangali maarufu Mdude kwa mahojiano kutokana na maneno yanayodaiwa kuwa ni ya uchochezi, walio yatoa.

Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi Agosti 12, 2023 na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Kamanda David Misime, imeleza kuwa watu hao walikamatwa jana maeneo ya Mikumi, mkoani Morogoro saa nne usiku.

“Kama ilivyoelezwa jana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Camillius Wambura, jeshi linawafuatilia ili liwakamate watuhumiwa walioandaa na kutoa maneno ya uchochezi, kazi hiyo inaendelea kufanyika kwa mujibu wa sheria,” amesema Misime katika taarifa hiyo.

Juzi IGP Wambura, aliwaonya watu wanaopanga kuandamana ili kuiangusha Serikali akisema wasijaribu kutingisha kiberiti kwa kuwa Polisi wapo imara kukabiliana nao.

Wambura alitoa onyo hilo, baada ya kusambaa kwa taarifa katika mitandao ya kijamii inayohusu kundi la watu wenye nia kuandaa maandamano nchi nzima ili kuiangusha Serikali kabla ya mwaka 2025 na kusisitiza kuwa kundi hilo linahusisha maandamano hayo na kushawishi Watanzania kuwaunga mkono na hoja zinazoendelea za bandari.

"Tuliamini hoja za bandari zinajibiwa kwa hoja, tukaamini baadhi ya watu walikwenda mahakamani basi wangeheshimu uamuzi wa mhimili huo, lakini badala yake wametoka na kutafuta ushawishi wa kuwachochea Watanzania kuwaunga mkono,” alisema IGP na kuongeza;

"Mmoja amekwenda mbali zaidi na kusema watahakikisha wanaiangusha Selikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kabla ya mwaka 2025. Nimewaita hapa kuwaambia wakome kabisa na kusitisha matamshi yao ya kichochezi na tutawachukulia hatua za kisheria."

Taarifa za kukatwa kwa watu hao, zilianza kusambaa leo alfajiri hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Alex Mkama, alijitenga nazo akisema: "Sijapata taarifa ya kukamatwa hao watu, kuna mwandishi mwenzako amenipigia pia kuniuliza hilo jambo, na nimefuatilia Kituo cha Mikumi ili kujua kama ni kweli, lakini wamesema hakuna mtu aliyekamtwa, nikipata lolote nitawapa taarifa."




Ilidaiwa kuwa Wakili Mwabukusi, Katibu wa Chadema Kanda ya Kati Emmanuel Masonga na Mdude Nyagali, wamekamatwa wakiwa katika gari moja ambapo walizuiwa katika kizuizi cha Mikumi na watu waliojitambulisha kuwa ni polisi.

Awali Katibu wa Chadema Mkoa wa Morogoro, Barnabas Okola, akizungumza na Mwandishi wa Mwananchi Digital kwa njia ya simu, alithibitisha kukamatwa kwa watu hao Mikumi, na kwamba viongozi wa mkoa walikuwa wanafuatilia suala hilo.

Okola ameiambia Mwananchi Digital kuwa wamefika Kituo Kikuu cha Polisi Morogoro ili kujua kama watu hao wamefikishwa hapo, hata hivyo walijibiwa kuwa hawapo, na kwamba labda wafuatilie kwingine.

"Ni kweli wamekamatwa Mikumi na kuna kiongozi wetu pale Mikumi tunawasiliana nae yuko Kituo cha Polisi Mikumi, amemuona Wakili Mwabukusi na amemkabidhi ufunguo wa gari yake na kumwambia ameambiwa anapelekwa chumba cha upelelezi kituoni hapo hivyo anasubiri," amesema Okola.

Amesema anaamini kuwa, kama Wakili Mwabukusi yuko kituoni hapo basi na wenzake watakuwa hapo.

Wakili Mwabukusi ni miongoni mwa mawakili wa walalamikaji katika kesi ya kupinga mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai (IGA), iliyokuwa imefunguliwa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya.

Kesi hiyo ya kikatiba namba 5 ya mwaka 2023 ilifunguliwa na mawakili wanne kutoka mikoa tofautofauti ambao ni Alphonce Lusako, Emmanuel Chengula, Raphael Ngonde na Frank Nyalus dhidi ya Serikali.

Hata hivyo Agosti 10, mwaka huu, Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya ilitoa uamuzi wa kesi hiyo ikisema mkataba huo hauna tatizo hivyo pingamizi lililowekwa na walalamikaji halina mashiko.