Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

IGP Wambura awaonya wanaotaka kuiangusha Serikali

Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Camillius Wambura

Muktasari:

Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Camillius Wambura amewaonya watu wanaopanga kuandamana ili kuiangusha Serikali akisema wasijaribu kutingisha kiberiti kwa kuwa polisi wapo imara kukabiliana nao.


Dar es Salaam. Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Camillius Wambura amewaonya watu wanaopanga kuandamana ili kuiangusha Serikali akisema wasijaribu kutingisha kiberiti kwa kuwa polisi wapo imara kukabiliana nao.

Wambura ametoa onyo hilo, baada ya kusambaa kwa taarifa katika mitandao ya kijamii inayohusu kundi la watu wenye nia kuandaa maandamano nchi nzima ili kuiangusha Serikali kabla ya mwaka 2025.

Wambura ametoa onyo hilo, leo Ijumaa Agosti 11, 2023 wakati akizungumza na wanahabari, ambapo amesema kundi hilo linahusisha maandamano hayo na kushawishi Watanzania kuwaunga mkono na hoja zinazoendelea za bandari.

"Tuliamini hoja za bandari zinajibiwa kwa hoja, tukaamini baadhi ya watu walikwenda mahakamani basi wangeheshimu uamuzi wa mhimili huo, lakini badala yake wametoka na kutafuta ushawishi wa kuwachochea Watanzania kuwaunga mkono,” amesema na kuongeza;

"Mmoja amekwenda mbali zaidi na kusema watahakikisha wanaiangusha Selikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kabla ya mwaka 2025. Nimewaita hapa kuwaambia wakome kabisa na kusitisha matamshi yao ya kichochezi na tutawachukulia hatua za kisheria," amesema Wambura.

Jana Agosti 10, Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya imetoa uamuzi mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai (IGA), ikisema hauna tatizo hivyo pingamizi lililowekwa na walalamikaji halina mashiko.

Pia, jana Alhamisi Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson wakati akizungumza na wananchi wa Jimbo la Mbeya Mjini aliwatahadharisha Watanzania kutokuunga mkono maandamano yaliyopangwa kufanyika nchi nzima kupinga uamuzi wa mahakama hiyo.

Wambura ambaye aliwahi kuwa Kamanda wa Polisi wa Manyara na Kinondoni, amesema uchochezi wanaofanya na uhaini ni makosa ya jinai na kwamba polisi haitakaa kimya, akisema jeshi halipo kimya na watawaonyesha watakaovunja sheria za nchi.

"Watanzania wawapuuze kwa kwa sababu nchi ni salama, wasikubali kushawishika kuingia kwenye maandamano, hatujawai kufika huko na hatutarajii kufika,” amesema na kuongeza;

"Jeshi letu la Polisi lipo imara wasitikise kiberiti, kama waliwahi kutikisa huko nyuma na kuguswa, wasiende huko wanakoshawishi kwenda, ni sehemu mbaya, wasijaribu kuendelea kufanya ushawishi na uchochezi."

Amesema kama kuna maneno ya kisiasa basi yajikite huko na siyo kutoka nje ya mstari, akisema polisi imeshuhudia maneno ya kutisha ya kichochezi yakiibuka ili kuweka ushawishi kwa Watanzania.

"Hivi tunavyongea zipo hatua zinazochukuliwa, maana hili jambo halivumiliki na halitakaa kuvumilika hasa ya uchochezi maana wamefika hatua mbaya sana...," amesema Wambura.