Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Polisi washikiliwa kwa uchunguzi kuchomwa moto kituo

Muktasari:

  • Kufuatia vurugu zilizopelekea kituo cha Polisi Mganza kuchomwa Moto watu kadhaa wakiwemo askari polisi wanashikiliwa kwa uchunguzi.

Chato. Watu kadhaa wakiwemo baadhi ya askari wa Kituo cha Polisi Mganza wanaodaiwa kuwa chanzo cha vurugu zilizotokea katika eneo hilo na kupelekea Kituo cha Polisi Mganza kuchomwa moto wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Geita kwa uchunguzi zaidi.

 Vurugu katika eneo hilo zilitokea Machi 30 baada ya wananchi kukataa kuuzika mwili wa Enos Misalaba baada ya msoma historia ya marehemu kudai alifariki kwa kuugua kifua kitendo kilichopingwa na waombolezaji waliamua kuurudisha mwili huo kituo cha Polisi.

Hata hivyo badaada ya kuzuka vurugu, zilisababisha polisi kutumia mabomu ya machozi kuwatuliza bila mafanikio na wananchi kuchoma moto kituo cha polisi.

Wananchi wa eneo hilo wanapinga uonevu unaofanywa na askari polisi wa kituo hicho wanaodawi kumkamata mtuhumiwa na kumpiga kitendo kinachodaiwa kusababisha kifo chake.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigella akizungumza kwenye mazishi ya Enos Misalaba (32) aliyepoteza maisha akiwa kwenye kituo cha afya Mganza alikokuwa akipata matibabu kwa madai ya kupigwa na askari akiwa mahabusu, Shigella amesema wanaoshikiliwa ni wale waliotajwa na wananchi kuwa chanzo cha tatizo.

Amesema Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya usalama vinashiriki kuhakikisha tatizo kama hilo halijirudii na tayari ameunda kamati ya kubaini chanzo pamoja na kilichosababisha kifo, majeruhi na kituo kuvamiwa sanjari na kujua waliohamasisha uvamizi.

“Wanaokuja hapa hawaji kutafuta mchawi au mhalifu wanakuja kutusaidia kutengeneza mfumo utakaotibu tatizo hili lisijirudie tena. Wapeni ushirikiano ni kwa manufaa yetu na manufaa ya Watanzania,” amesema Shigella.

Shigella amesema Serikali haimlindi mtu au kumtetea anayefanya mambo ya kona kona na kwamba ili kumaliza tatizo katika kata hiyo anaunda timu itakayohusisha vyombo vya usalama, Takukuru pamoja na wataalamu kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa ili kukomesha tabia ya watu kuonewa na kupoteza maisha.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa mkoa amelaani kitendo cha wananchi kujichukulia sheria mkononi na kuchoma kituo cha polisi na kusema kitendo hicho hakikubaliki kwani kinahatarisha usalama wa watu na kutaka wananchi watoe taarifa kwenye mamlaka pindi wanapoona jambo lisilo sawa kwenye jamii.

“Tujenge misingi ya utawala bora na utawala wa sheria mnapokuwa hamjaridhika na jambo msijichukulie sheria mkononi. Tuwasihi vijana jambo lililofanyika halikubaliki silaha zikiachwa hovyo zitakuja kusumbua mtaani niwaombe lililotokea lisijirudie tena.”