Osha yaanika mbinu kujenga Tanzania ya viwanda

Meneja wa wakala wa afya na usalama mahali pa kazi ‘Osha’ kanda ya Mashariki Jerome Materu amesema sheria ya afya na usalama mahali pa kazi isimamiwe .
Muktasari:
Materu amesema hayo wakati akifunga mafunzo ya afya na usalama mahali pa kazi yaliyoshirikisha kampuni 56 za uzalishaji na utoaji huduma kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro.
Morogoro. Meneja wa wakala wa afya na usalama mahali pa kazi ‘Osha’ kanda ya Mashariki Jerome Materu amesema sheria ya afya na usalama mahali pa kazi isimamiwe ili mkakati wa kuifanya Tanzania kuwa na uchumi wa viwanda ufanikiwe.
Materu amesema hayo wakati akifunga mafunzo ya afya na usalama mahali pa kazi yaliyoshirikisha kampuni 56 za uzalishaji na utoaji huduma kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro.
Amesema kuifanya nchi kuwa ya uchumi wa viwanda ni moja ya mikakati ya Rais John Magufuli na ili viwanda viweze kuzalisha kwa tija lazima sheria hiyo ya mwaka 2003 isimamiwe na kutekelezwa kikamilifu.
Sheria hiyo inataka kila kiwanda au kampuni ya uzalishaji na utoaji huduma kuhakikisha inaunda kamati za afya ili ziweze kutoa huduma ya kwanza na kutoa elimu ya namna ya kufanya kazi katika mazingira salama.
Kwa taarifa zaidi nunua gazeti lako la Mwananchi au soma mtandaoni kupitia www.epaper.mcl.co.tz