Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Omba msaada wa Mungu kuyashinda majaribu unayopitia

Mwalimu George Mbwambo kutoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Usharika wa Buza.

Bwana Yesu asifiwe. Nakukaribisha katika mahubiri ya siku ya leo. Mimi ni Mwalimu George Mbwambo kutoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Usharika wa Buza.


Zaburi 121:1-2

1.            Nitayainua macho yangu niitazame milima, msaada wangu utatoka wapi?

2.            Msaada wangu u katika Bwana, aliyezifanya mbingu na nchi.

Katika neno la Mungu tulilosoma hapo juu tumeona muimba Zaburi akizungumza hali ya mazingira aliyokuwa anapitia kwenye maisha yake, amesema ameyainua macho yake atazame milima na alipoiangalia milima hiyo akisema msaada wake utatoka wapi? Akajibu kwamba msaada wake u katika Bwana.

Biblia inapozungumzia milima mara nyingi inaelezea kuhusu majaribu. Hivyo basi, inawezekana muimba Zaburi alipitia majaribu ambayo hata alipotazama watu au jamii inayomzunguka haoni msaada wowote mpaka akafika hatua akasema msaada wangu upo katika Bwana.

Katika maisha tunayoishi duniani, yapo majaribu tumekutana nayo hata wakati mwingine tumetafuta mahali pa kupata msaada juu ya jaribu hilo unakosa. Majaribu hayo yanaweza kuwa magonjwa, hali mbaya ya kiuchumi, kukosa kazi na mengine mengi.

Leo nikutie moyo kwamba, Mungu anao msaada kwa ajili yako juu ya jaribu au changamoto unayopitia.

Katika kutambua namna ya kupokea msaada wa Mungu kwenye maisha yako tuangalie mifano ifuatayo:

Mfano 1. Mathayo 14; 28-30. Petro akamjibu, akasema Bwana ikiwa ni wewe niamuru nije kwako juu ya maji. Akasema njoo, Petro akashuka chomboni, akaenda kwa miguu juu ya maji ili kumwendea Yesu. Lakini alipoona upepo, akaogopa akapiga yowe akisema, Bwana niokoe.

Katika habari hii natamani kujifunza mambo yafuatayo:

  1. Petro kumuona Yesu juu ya maji akitembea na kumuomba naye aende juu ya maji.

Hapa unamuona Petro akitamani kutembea juu ya maji, lakini ikionyesha wazi si kwa nguvu zake bali kwa kumtegemea Mungu, “Alisema ikiwa ni wewe niamuru nije.’’ Akiwa na maana kwamba bila ya kuruhusiwa na Yesu asingeweza kutembea juu ya maji. Katika maisha ya kila siku unapotaka kuanza jambo lolote usianze kwanza kabla hujamshirikisha Mungu kwa sababu bila kumshirikisha Mungu jambo hilo linaweza lisifanikiwe.


  1. Petro kuuona upepo na kuanza kuzama, ukisoma vizuri habari hii kuanzia Mathayo 14:24 utagundua kuwa, wanafunzi wa Yesu walipoambiwa waende mpaka ng’ambo walipofika njiani chombo chao kilianza kupata shida kwa sababu ya upepo, hivyo wakati Petro anamuona Yesu naye kumwambia njoo juu ya maji, bado upepo ulikuwepo na Yesu alikuwa juu ya maji. Lakini Petro alianza safari bila kutazama upepo na macho yake yalikuwa yakimtazama Yesu peke yake. Hivyo hakuzama.

Kwenye safari ya maisha ya kila siku unapaswa kumtazama Yesu peke yake ili ufanikiwe na kustawi katikati ya changamoto unazokutana nazo, kwani changamoto hazikosekani ila unamuhitaji Yesu akusaidie katikati ya changamoto, maana yeye atazituliza au majaribu unayokutana nayo.


c) Petro akamuita Yesu wakati anapotaka kuzama naye alimsaidia.

Hapa tunajifunza kwamba, katikati ya bahari Yesu alikuwepo na ndiye aliyemwambia Petro njoo, lakini wakati Petro alipoanza kuzama Yesu hakumsaidia chochote mpaka alipoomba msaada, ndipo Yesu alimpatia msaada. Unapopitia changamoto au majaribu yoyote unahitaji kumuomba Mungu msaada ili ajue unatambua yeye ndiye msaada wako pekee.


Mfano 2. Luka 8:43-44 "…na mwanamke mmoja, ambaye ametokwa na damu muda wa miaka kumi na miwili (aliyekuwa amegharimiwa mali zake zote kwa kuwapa waganga) asipate kuponywa na mtu yeyote. Alikwenda nyuma yake, akaugusa upindo wa wazi lake na mara hiyo kutoka damu kwake kulikoma.”

Hapa natamani tujifunze mambo yafuatayo:

  1. Mwanamke aliyetokwa damu kutumia gharama kubwa bila kupata msaada.

Biblia inatuonyesha mwanamke huyu aliyotokwa damu alitumia mali nyingi ambazo bado hakupa msaada. Katika maisha haya yapo majaribu ambayo yanaweza kuja kwenye maisha yako na kutumia mali nyingi na muda mwingi lakini bado ukakosa msaada kabisa, kwani changamoto zingine unamhitaji Yesu pekee.

  1. Mwanamke aliyotokwa damu kwenda kwa Yesu kutafuta msaada akiwa peke yake. Unaposoma habari hii unagundua alipokwenda kwa waganga, alitumia mali zake zote zikaisha bila kupata msaada baadaye ndipo ameamua kwenda kwa Yesu kutafuta msaada. Nimetafakari sikuona mtu aliyempeleka kwa Yesu lakini kwa waganga kuna watu waliompeleka.

Mara nyingi unapokutana na majaribu au changamoto mwanzoni utaona watu wakijitokeza kukusaidia lakini changamoto au jaribu hilo likiwa la muda mrefu huoni mtu wa kukusaidia ni Yesu pekee ambaye hawezi kukuacha.

Lakini pia nimejifunza kwamba, mwanamke aliyetokwa damu angekutana na Yesu mapema asingetumia gharama kubwa za mali na muda alioupoteza, hivyo umekutana na tatizo au jaribu anza kumshirikisha Mungu kwanza.

Nakuombaea Mungu akupe msaada katika jaribu unalopitia.

Kwa maoni 0788 873 267