Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nape ashukuru kupona kwenye ‘panga’ la Samia

Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye wakati wa hafla ya ufunguzi wa jengo la Makao Makuu ya Umoja wa Posta Afrika (PAPU) lililopo eneo la Philips jijini Arusha.

Muktasari:

  • Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema baada ya kuona orodha ya uteuzi mpya akiwa safarini kuelekea Arusha, alimwambia dereva asimame pembeni kisha kuongeza AC ndani ya gari hilo ilia some kwanza mabadiliko ya Baraza la mawaziri.

Dar es Salaam. Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye ametumia dakika chache kumshukuru Rais Samia Suluhu kwa kuendelea kumuamini kuongoza wizara hiyo baada ya kumuacha katika mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri yaliyofanyika wiki iliyopita.

 Nape ametoa maelekezo hay oleo Septemba 2, 2023 wakati wa uzinduzi wa jengo la makao makuu ya Umoja wa Posta Afrika (PAPU) lililopo jijini Arusha, lililozinduliwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Uzinduzi wa jengo hilo umekwenda sambamba na uzinduzi wa stika mpya za posta kwa nchi za Tanzania, Algeria, Nigeria, Misri, Morocco, Senegal na Zimbabwe.

"Nilipokuwa nakuja Arusha Agosti 30 mwaka huu, nikiwa njiani katibu mkuu alinitumia mkeka, nilivyouna nilimuomba dereva asimame kidogo,” amesema Nape akifafanua:

“Niliongeza AC ya gari nikaanza kusoma hadi mwisho nikaona nimetoboa, nikaangalia Naibu wangu katoboa, Katibu Mkuu na Naibu Katibui Mkuu pia wametoboa.”

Kuhusu jengo hilo, Nape amesema ni hatua ya kutimiza ndoto za hayati Baba wa Taifa Hayati Julius Nyerere ambaye Januari 18, 1980 ilijitolea kuwa mwenyeji wa makao makuu ya Posta barani Afrika.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Mtendaji wa PAPU Sifundo Moyo alisema malighafi zote katika ujenzi wa jengo hilo la kisasa zimetoka Afrika na hivyo kuchangia kukuza uchumi ndani ya Afrika.

Mwenyekiti wa baraza la Utawala PAPU, amesema kukamilika kwa makao makuu ya umoja huo kutasaidia na uboreshwaji wa huduma za posta na mawasiliano Afrika na duniani.

Awali Waziri mpya wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa aliyezungumza katika mkutano huo baada ya kuapishwa siku chache zilizopita aliahidi wizara hiyo kuendelea na mpango wa kutatua migogoro ya ardhi kwa kupima maeneo yote yanayopaswa kupimwa.