Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mzee Asas afariki dunia

Mzee Asas afariki dunia

Muktasari:

  • Mwenyekiti wa Kampuni za Asas Group, Alhaj Faraj Ahmed Abri amefariki dunia Leo Ijumaa Agosti 13, afajiri, akiwa Jijini Dar es Salaam.

Iringa. Mwenyekiti wa Kampuni za Asas Group, Alhaj Faraj Ahmed Abri amefariki dunia leo Ijumaa Agosti 13 alfajiri, akiwa jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika familia hiyo, Mzee Abri ambaye ni baba mzazi wa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Salim Abri Asas, maziko yatafanyika leo baada ya Swala ya adhuhuri katika makaburi ya Kisutu Dar es Salaam.

"Hakutakuwa na mikusanyiko kwa tutakaokuwa Iringa, tafadhali tutumie zaidi teknolojia za habari kutoa pole na shughuli nyingine," ilieleza taarifa hiyo.

Mwenyekiti wa CCM, Manispaa ya Iringa Said Rubeya alithibitisha taarifa hiyo na kutoa pole kwa familia, wafanyakazi wa Asas, ndugu jamaa na marafiki.

"Kama tulivyo shauriwa tutumie teknolojia ya habari na mawasiliano kuomboleza, nitoe pole nyingi kwa familia, pole pia kwa M NEC wetu, Salim Asas. Hakika kwa Mwenyezi Mungu ni marejeo," alisema Rubeya.

Imeandikwa na

Tumaini Msowoya, Mwananchi