Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwinyi: Bima ya Takaful kuitangaza Zanzibar kiuwekezaji

Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi akizungumza wakati wa kuzindua bima inayofuata misingi ya Kiislamu ya Takaful  Mjini Unguja.

Unguja. Rais wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi amesema kuanzishwa bima inayofuata misingi ya Kiislamu (Takaful) kwa Zanzibar ni fursa kwa nchi kujitangaza kama eneo bora la uwekezaji kwa mwambao wa Afrika Mashariki.

Amesema Zanzibar imeweka misingi imara kuhakikisha inatoa fursa kwa kampuni na watu binafsi kupata huduma mpya ya Takaful.

Dk Mwinyi ametoa kauli hiyo leo Julai 5, 2023 wakati akizindua huduma ya bima inayofuata misingi ya Kiislamu itayotolewa na Kampuni tanzu ya Shirika la Bima la Zanzibar (ZIC) ijulikanayo kama ‘ZIC Takaful.’

“Natumia hadhara hii kuwakaribisha wawekezaji wa ndani na nje ya nchi yetu kuchangamkia fursa hii kwa kuja kuwekeza katika huduma za bima za aina hii kuongeza uwezo wa kukatia bima miradi mikubwa itakayochochea ukuaji wa uchumi wetu,” amesema Dk Mwinyi

Alisema, huduma ya ‘Takaful’ tayari inatumiwa na nchi nyingi barani, Ulaya na Asia katika kutoa fursa kwa biashara mbalimbali zinazofuata misingi ya Kiislamu kupata huduma za bima zenye miongozo ya Uislamu.

Amesema Zanzibar ina kazi kubwa ya kufanya ili kuongeza kasi ya kufikisha huduma za bima kwa wananchi waliopo maeneo ya mbali mijini na Vijijini, ikiwa ni pamoja na utoaji wa elimu sambamba na kubuni njia mbalimbali ili kuwafikia wananchi wanaohitaji huduma hiyo.

Naye, Mkurugenzi Mwezeshaji wa ZIC, Afarat Ali Haji alieleza lengo la kuanzishwa kwa huduma za Takaful Zanzibar ni kuwapa uhuru wananchi kuchagua huduma bora na kupata suluhisho la kukata bima isiyo na riba sambamba na kukuza uchumi na maendeleo ya jamii na kujengea taswira njema kwa taifa.

Amesema huduma ya bima ya ‘Takaful’ mbali na kukuza na kuongeza mitaji pia ina changia katika kuongeza jitihada za kuanzisha bima ya maisha hapo baadaye, baada ya kuimarika kwa huduma za Takaful nchini, hivyo, aliiomba Serikali kuwaongezea mtaji wa kufanikisha huduma hizo.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (Tira) Dk Baghayo Saqware amesema sekta ya bima imepunguza umasikini nchini kwa kuisaidia jamii kukuza biashara zao.

Kampuni tanzu ya ‘ZIC TAKAFUL’ ni kampuni inayotoa huduma za bima kwa kufuata misingi ya Sheria za Kiislamu Zanzibar