Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwanafunzi Udom afariki dunia mafunzoni Udzungwa

Muktasari:

  • Mwili wa mwanafunzi huyo aliyezama katika maporomoko ya maji Sanje ulitolewa kwenye maji na wataalamu wa kuogelea na taratibu nyingine za uchunguzi zinaendelea.

Morogoro. Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linachunguza taarifa ya kifo cha mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), Hezekiel Petro (21) aliyekufa maji kwenye maporomoko ya maji Sanje yaliyopo Hifadhi ya Taifa ya Udzungwa, Kata ya Sanje, Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Jumatatu, Desemba 23, 2024 mjini hapa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama amesema tukio hilo limetokea jana Jumapili, Desemba 22, 2024.

Kamanda Mkama amesema Hezekiel, aliyekuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika chuo hicho akisomea masomo ya sanaa na historia, alikufa maji baada ya kukanyaga jiwe lenye utelezi na kutumbukia kwenye maji yenye kina kirefu.

"Tunachunguza tukio la Hezekiel Petrol, aliyefikwa na mauti baada ya kukanyaga jiwe lenye utelezi na kutumbukia katika maji yenye kina kirefu na kupoteza maisha wakati alipotembelea Hifadhi ya Idzungwa na wanafunzi wenzake kwenye ziara ya mafunzo kwa vitendo," amesema Kamanda Mkama.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Alex Mkama

Kamanda Mkama amesema wanafunzi zaidi ya 300 wakiwa wameambatana na wakufunzi wao walikuwa kwenye ziara ya mafunzo kwa vitendo eneo hilo.

Kutokana na tukio hilo, Jeshi la Polisi limetoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari na kufuata maelekezo ya wataalamu wanapotembelea maeneo yenye upekee.