Mwanafunzi kidato cha kwanza abakwa hadi kufa
Muktasari:
- Watu watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro kwa tuhuma za kubaka hadi kufa mwanafunzi wa kidato cha kwanza Shule ya Sekondari Mkwasa.
Hai. Watu watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro kwa tuhuma za kubaka hadi kufa mwanafunzi wa kidato cha kwanza Shule ya Sekondari Mkwasa.
Akizungumza leo Jumatatu Juni 28, 2021 Kamanda wa Polisi mkoani humo, Amon Kakwale, amesema tukio hilo limetokea jana Jumapili Juni 27, 2021 katika kijiji cha Mungushi Kati Wilaya ya Hai.
Amemtaja mwanafunzi huyo kuwa ni Sayuni Ruben (14), “huyu binti alikutwa amefariki baada ya watuhumiwa kuutupa mwili wake baada ya kumbaka.”
Amesema Juni 26, 2021 binti huyo aliondoka nyumbani kwao na kwenda katika kanisa la Lutherani Mungushi kwa ajili ya maandalizi ya sherehe ya vijana.
Amesema wakati mwanafunzi huyo anarudi nyumbani saa 1:30 usiku alikutana na watu hao waliombaka.