Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwanafunzi darasa la pili apotea siku sita, mwili wake wakutwa jumba linalojengwa

Muktasari:

Polisi Mkoa wa Pwani nchini Tanzania linaendelea na msako wa kuwatafuta watuhumiwa waliohusika na kifo cha mwanafunzi wa darasa la pili kutoka shule ya msingi Jitegemee Wilaya ya Kibaha mkoani huo aliyekutwa amefariki ndani ya jumba ambalo ujenzi wake haujakamilika.

Kibaha. Mwanafunzi aliyekuwa anasoma  darasa la pili Shule ya Msingi Jitegemee Halmashauri ya Mji wa Kibaha Mkoa wa Pwani nchini Tanzania (jina linahifadhiwa kwa sasa) amekutwa amekufa ndani ya nyumbani ambayo ujenzi wake bado haujakamilika.

Mwanafunzi huyo ambaye inadaiwa alipotea tangu Januari 14, 2020 na taarifa zake kutolewa na ndugu kwa Jeshi la Polisi mkoani Pwani inaelezwa mwili wake umekutwa na michubuko sehemu za siri tukio ambalo linaleta hofu kuwa huenda alifanyiwa vitendo vya ubakaji kabla ya kuuawa.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani, Wankyo Nyigesa amesema awali kabla ya tukio hilo mwanafunzi huyo aliondoka nyumbani kwao akiwa na shangazi yake, Agnes Peter kwenda gulioni maeneo ya Mwendapole kwa shughuli za biashara.

Wankyo amesema ilipofika saa 12 jioni,  shangazi yake huyo alimruhusu marehemu kwenda nyumbani akiwa peke yake kwaajili ya kufanya maandalizi ya shughuli za siku inayofuata.

Amesema shangazi yake alipofunga biashara zake na kurejea nyumbani hakumkuta marehemu na kuchukua hatua ya kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi juu ya tukio hilo pamoja na maeneo mengine ambapo jitihada za kumtafuta ziliendelea bila mafanikio hadi kukuta miwili wake ukiwa ndani ya jumba hilo juzi Januari 19,2020.

Amesema Jeshi la Polisi linaendelea kuwasaka watu waliohusika na kitengo hicho ili hatua stahiki zichukuliwe dhidi yao.

Polisi wamesema kwa sasa hawawezi kutaja jina la marehemu hadi hapo baadaye uchunguzi wao utakapokamilika.