Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwalimu aliyetoweka Simiyu akutwa amefariki Musoma

Mwalimu Monica Patrick enzi wa uhai wake.

Muktasari:

  • Mwalimu Monica Patrick (31) mkazi wa Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu aliyetoweka katika mazingira ya kutatanisha amepatikana akiwa amekufa na mwili wake kutelekezwa kichakani mtaa wa Nyang'wena Manispaa ya Musoma.

Musoma. Mwalimu wa Shule ya Msingi Lagangabilili Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu, Monica Patrick (31) aliyetoweka katika mazingira ya kutatanisha amepatikana akiwa ameuwawa na mwili wake kutelekezwa kichakani mtaa wa Nyang’wena Manispaa ya Musoma.

 Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Mara, Agostino Magere amethibitisha mwili huo kuopolewa kutoka kwenye kichaka kilichoko ndani ya maji pembezoni mwa Ziwa Victoria.

 “Februari 19, 2023, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mara tulipokea taarifa ya mwili wa mtu kuonekana ikielea juu ya maji kwenye kichakani kilichopo mtaa wa Nyang’wena Manispaa ya Musoma na kweli tullipofika tuliukuta na kuuopoa ukiwa umeharibika.

“Marehemu ametambulika kwa jina la Monica Patrick aliyekuwa mwalimu katika shule moja ya msingi mkoani Simiyu,” amesema Kamanda Magere

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu Februari 20, 2023, Kamanda huyo wa Zimamoto na Uokoaji amesema mwili wa Mwalimu Monica umekabidhiwa kwa wataalam wa afya kwa uchunguzi zaidi kubaini chanzo cha kifo chake.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Nyang’wena, Selemani Makanja amesema taarifa za awali zinadai Mwalimu Monica ambaye ndugu zake wametoa tangazo la kutoweka kwake kupitia njia ya mitandao ya kijamii alifariki dunia baada ya kunyweshwa dawa na mtu anayeaminika kuwa ni mganga wa kienyeji kwa lengo la kufanikiwa kibiashara.

“Inasemekana marehemu ambaye pia tumeelezwa kwamba ni mwalimu huko mkoani Simiyu alikwenda kwa mganga huyo kwa lengo la kuaguliwa ili afanikiwe katika biashara yake ya madini. Tunasubiri taarifa za uchunguzi kujua chanzo cha kifo,” amesema.

Amesema mwili wa merehemu Monica umekutwa eneo la mradi wa majitaka ambao haujakamilika, huku akiiomba Serikali kukamilisha mradi huo kuondoa kichaka ambacho kimegeuka kuwa

Kupitia mitandao ya kijamii, familia ya Mwalimu Herman Mlale wa Sanya Juu Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro ilitangaza kutoweka katika mazingira ya kutatanisha kwa mtoto wao Monica Patrick, ikiomba mwenye taarifa ama kuwasiliana na familia hiyo kupitia namba tatu za simu zilizoambatana na tangazo hilo au kituo chochote cha polisi.

Taarifa zilizoifikia Mwananchi zinaeleza kuwa mwili wa Mwalimu Monica tayari umewasili nyumbani kwao Sanya Juu ambako mazishi yanatarajiwa kufanyika leo kutokana kuharibika.

Taarifa ambazo hazijathibitishwa zinadai mwalimu Monica ambaye haijajulikana iwapo alikuwa akijihusisha ba biashara ya madini kama inavyoelezwa baada ya kifo chake, alitoweka muda mfupi baada ya kupokea fedha za mkopo kiasi cha Sh5 milioni kutoka katika moja ya taasisi za fedha mkoani Simiyu.